Posts
Showing posts from March 5, 2018
Fahamu Madhara Ya Usukaji Wa Nywele Bandia Na Uvaaji Wa Mawigi
- Get link
- X
- Other Apps
Katika karne ya sasa , uvaaji wa wigi umekuwa fasheni katika sekta ya urembo na hutumika hususan na wanawake. Ingawa uvaaji wa wigi huwafanya wanawake hao kuonekana ni walimbwende zaidi. Wigi huvaliwa zaidi na kinamama wenye asili ya Afrika au Wamarekani wa asili ya Afrika. Lakini tukiangalia moja ya chimbuko hasa la uvaaji wigi ni ubaguzi uliokuwepo wakati wa utumwa ambapo wale wenye ngozi nyeupe na nywele shombeshombe walipewa kazi za ndani na wale wasio na ngozi nyeupe na nywele zisizo shombeshombe walifanyishwa kazi ngumu za mashambani. Watumwa waliopelekwa barani Amerika hawakuweza kuzihudumia nywele zao kutokana na hali ngumu, na mabwenyenye waliwashusha hadhi na kuwavunja moyo kwa kuwaambia hawakuwa na nywele bali ni "manyoya". Lakini sababu nyingine inayodhaniwa kuwaathiri wanawake wa asili ya Afrika ni fikra kuwa mwanamke mwenye nywele ndefu pengine hadi mgongoni ni mrembo zaidi. Pia siku hizi warembo na wanaoshiriki katika mashindano ya urem...
Ikulu Yakanusha Taarifa Dhidi Ya Waziri Hamis Kigwangala
- Get link
- X
- Other Apps
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa amekanusha kuwa Rais Magufuli kutengua uteuzi wa Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala kwa mujibu wa barua inayosambaa kwenye mitandao kuwa ni uzushi na imetengenezwa na wahalifu. Alichokisema Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa. Barua inayosambaa kwenye mitandao ambayo imetengenezwa na wahalifu.
DIAMOND KULAMBA SHAVU KOMBE LA DUNIA SIRI YAFICHUKA!
- Get link
- X
- Other Apps
DAR ES SALAAM: Nyuma ya tukio la Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kulamba shavu la kuimba wimbo wa uzinduzi wa Michuano ya Kombe la Dunia 2018, Ijumaa Wikienda limebaini siri iliyochangia uteuzi wake huo. Katika uchunguzi mdogo uliofanywa na gazeti hili, mambo matatu makubwa ambayo ndiyo sababu kubwa iliyowafanya waandaaji wampe kipaumbele rais huyo wa Wasafi Classic Baby (WCB). Ijumaa Wikienda lilibaini kuwa, jambo la kwanza lililochangia Diamond ateuliwe ni bidii ya uongozi wake chini ya Sallam SK. Sallam ametajwa kuwa miongoni mwa mameneja ambao wana ‘connection’ nyingi za vituo vikubwa vya redio na televisheni ambavyo hucheza nyimbo za Diamond duniani. Ilielezwa kuwa, connection hizo ndizo zilizochangia kuwashawishi waandaaji wa michuano hiyo wakati walipokuwa wanaangalia ni wasanii gani wa Afrika ambao wana uwezo na ushawishi mkubwa, wakampendekeza Diamond. Mbali na hilo, jambo lingine lililochangia Diamond ateuliwe na kushiriki katika uzinduzi wa mashindano ...
BREAKING NEWS : AJALIMBAYA DALADALA YAGONGANA NA GARI LA TAKA,LASABABISHA VIFO NA MAJERUHI DODOMA
- Get link
- X
- Other Apps
Watu sita wamefariki dunia papo hapo huku wengine sita kujeruhiwa vibaya baada ya basi la abiria walilokuwa wakisafiria kugongana na lori mkoani Dodoma. Eneo la ajali ambapo watu sita wamefariki baada Akithibitisha taarifa hizo Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma, Gillece Muroto amesema ajali hiyo imetokea leo Jumapili Machi 4, 2018 majira ya mchana ambapo daladala aina ya Toyota Hiace iliyokuwa na abiria kugongana na lori la kubebea taka. Taarifa zaidi nitazitoa baada ya kufuatilia lakini kwa ufupi ajali hiyo ipo na watu sita wamekufa na wengine sita wapo katika hospitali ya rufaa ya mkoa na hali zao sio nzuri,” amesema Muroto kwenye mahohjiano na Gazeti la Mwananchi.
Kilimo Bora Cha Viazi Vitamu
- Get link
- X
- Other Apps
Viazi vitamu ni moja kati ya mazao makuu ya mizizi nchini Tanzania ambalo hulimwa kwa ajili ya chakula. Zao hili ni moja kati ya mazao ya kinga ya njaa kutokana na sifa yake ya kuvumilia ukame. Zao la viaViazi vitamu, asilia yake ni Amerika ya Kati na ya Kusini. Nchini Tanzania, zao hili hulimwa zaidi katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Dodoma, Morogoro,Kagera,Arusha na Ruvuma. Viazi vitamu hutumika kama chakula kwa kutayarishwa katika njia mbalimbali kama vichembe, na Matobolwa. Pia Unga wa viazi vitamu hutumika kutengeneza vyakula kama keki, maandazi, kalimati na tambi. Majani ya viazi huliwa kama mboga pia hutumika katika kutayarisha mboji. Aina za viazi vitamu Kuna aina nyingi za viazi vitamu zinazolimwa ulimwenguni. Hapa nchini Tanzania aina zinazolimwa zaidi ni Ukerewe, Simama, Kakamega, Karoti C, Mwananjemu, Ali mtumwa mayai, Mavuno, Pananzala, Kibakuli, Sinia,Vumilia na Polista. Faida: vina wanga, vitamin, kambalishe, madini ya kalisiuamu, potasiamu, chu...
Breaking News: Moto Waunguza Shule ya Wasichana Korogwe
- Get link
- X
- Other Apps
Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe iliyoko wilayani Korogwe Mkoa wa Tanga, inaungua moto usiku huu, huku chanzo cha ajali ya moto huo kikiwa hakijajulikana. Inadaiwa watu kadhaa wamejeruhiwa kutokana na moto huo. Hakuna vifo vilivyoripotiwa ama kuthibitishwa hadi sasa. Tunaendelea kufuatilia kwa kina, taarifa zaidi tutakuletea baadaye.