Dogo Janja, Uwoya wamwagana rasmi? Madee atoa majibu
Kufuatia kusambaa kwa taarifa za kumwagana chini kwa wanandoa mastaa, Dogo Janja na Irene Uwoya, Baba wa muziki wa Janjaro, Madee amekanusha tetesi hizo akiziita ni uvumi na kwamba wawili wao hawana tatizo lolote. Stori za mastaa hao kumwaga zimezidi kuenea zaidi siku za hivi karibuni zikichagizwa na kitendo cha Uwoya kutoonekana Hospitalini alipokuwa amelazwa Janjaro ambaye anaumwa. " Hakuna taarifa kama hizo, Janja na Uwoya wapo kama kawaida hawajatemana kama ambavyo inaenezwa, hizo ni tetesi tu au niite ni uzushi, nachokuambia wale bado ni mtu na mke wake hizo stori za kuachana mnazipika nyie," amesema Madee. Lakini leo Uwoya alizidisha kasi ya watu kuamini kuwa hakuna ndoa baina ya wawili hao baada ya kujibu comment ya shabiki wake kwenye Instagram aliyeandika, " Dogo Janja atakufa Irene" kisha Uwoya kujibu, " hapana, simlisema wenyewe nitafute wa umri wangu yeye bado mdogo? sasa nimefuata ushauri jamani...au kashakua?" Masta...