Posts

Showing posts from December 9, 2014

BREAKING NEWS: WAJERUHIWA KATIKA VURUGU DUMILA.

Image
WATU kadhaa wamejeruhiwa katika vurugu zilizotokea jioni hii huko Dumila mkoani Morogoro kati ya wakulima na wafugaji ambapo polisi wameingilia kati na kutumia mabaomu ya machozi kutuliza ghasia hizo.  Chanzo cha vurugu hizo kinadaiwa kuwa ni kukatwa mkono kwa mkulima mmoja aishiye Kijiji cha Mketeni wilayani Kiloasa wakati akibishana na mfugaji ambaye ni kabila la Kimasai kuhusu eneo la kulishia mifugo.  Kufuatia kitendo hicho cha kukatwa mkono, mkulima huyo aliwafuata wenzake na kuwapa taarifa ambapo walikusanyika na kuanzisha vurugu dhidi ya wafugaji wa eneo hilo.Baada ya kuona kuwa bado haitoshi na baadhi ya wafugaji kukimbia, wakulima walimalizia hasira zao katika Barabara ya Morogoro - Dodoma ambapo waliamua kuifunga kwa takribani masaa mawili huku wakichoma matairi Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) waliingilia kati na kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wakulima ambao pia walikuwa tayari wamevamia baadhi ya nyumba za kulala wageni z...

DUNIA IMEKWISHA: BINTI AKUTWA AKIFANYA JARIBIO LA KUMLA MTOTO WAKE BAADA YA KUJIFUNGUA!

Image
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Li Zhenghua 24, amekutwa akifanya jaribio la kumla Mtoto wake aliyejifungua siku chache zilizopita, baada ya kumkuta taya yake ikiwa imenasa kuzunguka Mkono wa Mtoto wake.  Tukio hilo la ajabu lilitokea katika Hospitali iliyoko Shenzhen Kusini mwa jimbo la Guangdong, China ambapo mwanamke huyo alifikishwa kujifungua na baadaye wahudumu wa Hospitali kufanya jitihada za kutafuta ndugu zake.  Hata hivyo mwanamke huyo akiwa na siku ya tatu Hospitalini hapo alikutwa na nesi akiwa katika jaribio la kumng’ata mtoto ambapo madaktari walitumia nguvu na kufanikiwa kumuokoa mtoto huyo ambaye tayari alikuwa na jeraha mkononi.

MAADHIMISHO YA MIAKA 53 YA UHURU WA TANZANIA BARA YAFANA JIJINI DAR LEO

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mikono wananchi waliofurika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam katika Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara akiwa katika Gari maalum liliozunguuka katika uwanja huo leo.Kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama,Jenerali Davis Mwamunyange. Vikosi vya Ulinzi na Usalama vikitoa salamu ya heshma wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alipowasili katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam leo katika sherehe za kilele cha maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua Gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama lilioandaliwa katika sherehe za kilele cha Maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika leo katika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mri...

BILIONEA EMAMI WA NIGERIA AMPATIA TAYO DOLA 350,000/= KAMA BACKUP BAADA YA KUSHINDWA KWENYE SHINDANO LA BBAHOTSHOTS

Image
Ndugu wasomaji wetu tunaomba support yenu kwa kutangaza nasi hapa kwenye hii blog kwa bei nafuu ili tuweze kuendelea kutoa habari bila tatizo lolote. Wasiliana nasi kupitia namba +255765957698 au email: pharsnyanda@gmail.com .  Tunashukuru kwa ushirikiano wenu. Mshindi wa pili wa  BBAHotshots, Tayo Folarin   Baada ya East Africa yote kuinua shangwe kubwa siku ya Jumapili Desemba 7 kusherehekea ushindi wa nguvu alioupata Mtanzania   Idris   kwenye  BBAHotshots , kulikuwa na story kwenye mitandao ya kijamii ambazo hazikuwapendeza watu wengi kwani ilionekana kama baadhi ya watu kama Nigeria hawakuwa na amani kuukosa ushindi huo na kuuona ukija Tanzania. Bilionea  Ayiri Emami Sasa mpya kutoka Nigeria ni kwamba bilionea mmoja hakupendezwa kumuona mwakilishi wao Tayo akiambulia patupu, bilionea huyo  Ayiri Emami  amempatia  Tayo Folarin  pesa ambazo ni zaidi hata ya kiwango ambacho kimetolewa na  BBAHots...