Posts

Showing posts from December 30, 2017

Dk. Shika Atangaza Kuihama Tanzania, Anaelekea Wapi? Soma Hapa

Image
MAPYA TENA! Dkt. Louis Shika ambaye amejipatia umaarufu baada ya kutangaza dau la kununua nyumba za Lugumi, amesema kwamba hivi karibuni anatarajia kwenda kusihi Marekani, baada ya Umoja wa Mataifa kumpandisha cheo. Akizungumza kwenye kipindi cha Weekend Breakfast cha East Africa Radio, Dkt. Shika amesema awali alikuwa anafanya kazi kwenye shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi (UNHCR) na sasa amepandishwa cheo, hivyo hata ofisi zake hazitakuwa tena Nairobi nchini Kenya, kwani zitahamishiwa New York Marekani. “ Sasa hivi nina mpango wa kusajili kampuni yangu halafu mimi nisepe, nikiwa hapa nchini nanyanyasika, nilikuwa nafanya kazi na Umoja wa Mataifa  Bara la Afrika, sasa ni world wide, ofisi itakuwa New York , nimepandishwa cheo, nafaya kazi ofisi ya UNHCR. “Hata mama Kevela alipogundua mimi ni balozi akasema nyinyi ndio mnaoongoza nchi hii, na watu wajue kuwa uteuzi wangu haukutokea Tanzania, nimeteuliwa kwa veto power, hizi

ELIMU YA BURE KWA WENYE MAGARI NA JINSI YA KUNUNUA MATAIRI YA GARI YAKO

Image
Hata kama huna gari kwa sasa naamini katika moja ya ndoto zako ni kumiliki gari, Isomee hii itakusaidia wewe na ndugu zako kama sio na rafiki zako. Matairi ya gari muda wake rasmi wa matumizi ni miaka minne ( 4 ) tu toka yatengenezwe (Sio toka uyafunge kwenye gari lako).......Ikishapita miaka minne toka tairi litengenezwe linaweza kupasuka wakati wowote. Jinsi ya kutambua tairi lilitengenezwa lini tafuta alama kwenye tairi iliyoandikwa kwa mfumo huu (*2603*) kuna kuwa na alama ya nyota mwanzo na mwisho wa hizo namba nne. Namba mbili za kwanza zinaonyesha tairi lilitengenezwa wiki ya ngapi katika wiki 52 za mwaka na namba mbili za mwisho zinaonyesha mwaka tairi lilipo tengenezwa. Kwa mfano *2603* inamaanisha tairi lilitengenezwa wiki ya 26 ya mwaka 2003 au *2699* inamaanisha tairi lilitengenezwa wiki ya 26 ya mwaka 1999. KAGUA MATAIRI YAKO USITUMIE TAIRI LILILO PITA ZAIDI YA MIAKA MINNE KWANI LINAWEZA PASUKA WAKATI WOWOTE......hapo ndio inapotokea tairi mpya umenu

ALICHOKIANDIKA MKE WA KAFULILA BAADA YA KUONANA NA TUNDU LISSU LEO

Image
Leo December 30, 2017 Mke wa aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila ambaye pia ni Mbunge wa viti maalum Singida  Jesca Kishoa   alikuwa Nairobi Kenya ambapo alienda kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu aliyeshambuliwa kwa risasi akiwa nyumbani kwake Dodoma na watu wasiojulikana. Kupitia account yake ya Instagram aliandika jumble usemao.>” Shauku yake ya kulitetea taifa hili imeongezeka mara 100000000000….. Aisee ni kama kuzima moto kwa petrol. Wasiojulikana wamemfanya awe jasiri zaidi.Glory to the Almighty God.Aluta Continua “

TRA Kumchunguza Kakobe Baada ya Kusema Ana Pesa Nyingi Kuliko Serikali

Image
Kufuatia Kauli ya Askofu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zakary Kakobe kudai kuwa ana pesa nyingi kuliko serikali, mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wamepanga kumchunguza kiongozi huyo wa dini. Hayo yamesemwa leo na Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo amesema; “Tupokea kauli ya Askofu Kakobe kwa unyenyekevu mkubwa sana kwa kuwa wao wanapenda watu wenye pesa nyingi ili waweze kupata haki yao “Kama mtu ana hela kuliko serikali, kama ambavyo tunajua serikali yetu inatoa huduma inanunua ndege, imejenga standard gauge, inajenga barabara, inatoa elimu bure, inalipa mishahara kwa watumishi wa umma, inalipia madawa hospitalini, inalipa na kutoa huduma za ulinzi na usalama kwa wananchi. Lakini Serikali hiyo tunaambiwa inazidiwa hela na Askofu Kakobe basi ni jambo jema. “Tunawafahamu matajiri wanalipa kodi, baada ya kauli ya Askofu Kakobe tukaanza kupitia kumbukumbu zetu ili kuona namna Askof

EBITOKE TENA,AIBUKA NA MENGINE KUHUSU BEN POL,AFUNGUKA MENGI LIVE

Image
Mchekesha kutoka kundi la Timamu, Ebitoke amefunguka uhusiano wake na msanii wa RnB Ben Pol ulivyo kwa sasa mara baada ya kupitia drama za hapa na pale. Ebitoke amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio kuwa licha ya kutofautiana hapo awali kwa sasa mapenzi yao yanaendelea kama kawaida. Hapana sijaachana naye, baada ya kulalamika kuwa hapokei simu yangu sasa hivi tupo vizuri kabisa, mlikuwa mnatuona hata kwenye baadhi ya show zake tupo pamoja, sasa hivi tupo fresh yeye ndiye boyfriend wangu sina mwingine,” alisema Ebitoke. Uhusiano wa wawili hawa ulianza June mwaka huu mara baada ya Ebitoke kujitokeza katika mitandao na vyombo vya habari na kudai kuwa anavutiwa na Ben Pol na angetamani kuwa naye katika mahusiano ya kimapenzi kitu ambacho kinaelezwa kilikuja kutimia hapo baadaye.

TCRA YASHUSHA GHARAMA ZA MAWASILIANO

Image
Mamlaka ya Mawasiliano nchini Tanzania (TCRA), imetangaza kupunguza kiwango cha gharama za mawasiliano ya simu nchini Tanzania kutoka 26.96 kwa dakika moja mwaka huu hadi 15.60 kuanzia 2018. Akitangaza punguzo hilo la viwango vipya vya mawasiliano ya simu ambavyo vitaanza kutumika Januari Mosi, 2018, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Kilaba amesema viwango hivyo vitaendelea kupungua kila mwaka hadi kufikia shilingi 2 mwaka 2022 Aidha Mhandisi Kilaba amesema hatua hiyo itasaidia kuongeza idadi ya watumiaji wa matumizi ya simu na kuongeza pato la watoaji huduma wa mitandao ya simu na taifa kwa ujumla.