MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZUNGUMZA NA WAJUMBE WANAWAKE WA MKUTANO MKUU WA CCM MJINI DODOMA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wajumbe Wanawake wa Mkutano Mkuu wa CCM mjini Dodoma ambapo aliwasihi kuendelea kudumisha umoja na mshikamano pamoja na kujishughulisha na shughuli mbali mbali za kiuchumi na kujiunga na Mabaraza mbali mbali ya kuwezesha wanawake. Baadhi ya Wajumbe walishindwa kujizuia na kuamka kwa shangwe na vifijo. Mke wa Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ,wilaya ya Lindi Mama Salma Kikwete akizungumza na Wajumbe Wanawake wa Mkutano Mkuu wa CCM mjini Dodoma . Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Dk. Tulia Ackson akungumza kwenye mkutano uliowakutanisha Wajumbe Wanawake wa Mkutano Mkuu wa CCM pamoja na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan mjini Dodoma. Sehemu ya Wajumbe waliohudhuria. Makamu wa Rais wa Jamhuri...