Posts

Showing posts from June 10, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AMUAPISHA JAJI WA MAHAKAMA YA RUFANI PAMOJA NA JAJI KIONGOZI, PIA AAGANA NA BALOZI WA OMAN ANAYEMALIZA MUDA WAKE HAPA NCHINI.

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Jaji Ferdinand Leons Katipwa Wambali kuwa Jaji Kiongozi, Ikulu Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Jaji Shaaban Ali Lila kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Jaji Shaaban Ali Lila mara baada ya kumuapisha kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Jaji Ferdinand Leons Katipwa Wambali mara baada ya kumuapisha kuwa Jaji Kiongozi, Ikulu Jijini Dar es Salaam. Read more »  

Kesi ya Bosi wa TRA na Wenzake Yarudishwa Tena Mahakama Kuu

Image
                 Mahakama ya Rufani Tanzania, imeamuru jalada la kesi inayomkabili Kamishna Mkuu wa zamani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya na wenzake kurudishwa Mahakama Kuu kwa ajili ya kusikilizwa rufani ya Jamhuri. Pia, imeagiza jalada hilo lipangiwe kusikilizwa kwa jaji mwingine dhidi ya rufaa ya kupinga kuondolewa shtaka la utakatishaji fedha katika kesi ya kujipatia Dola za Marekani milioni 6. Hukumu hiyo ilisomwa jana na Msajili wa Mahakakama ya Rufani, Zahra Maruma baada ya kusikilizwa na jopo la majaji watatu, likiongozwa na Mwenyekiti Salum Masati akisaidiana na Kipenka Musa na Augustine Mwarija. Msajili Maruma alisema mahakama hiyo imeona kwamba Jaji Mfawidhi Moses Mzuna alikosea kukubali pingamizi la utetezi na kutupilia mbali kusikiliza rufani ya kupinga uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wa kuliondoa shtaka la kutakatisha fedha dhidi ya Kitilya na wenzake. “Mahakama hii imebatilisha uamuzi uliotolewa na Jaji Mzu

Pichaz: Muhammad Ali Alivyoagwa Kiislamu

Image
                  Maombi ya Kiislamu ya kuswaliwa kwa jeneza la marehemu bondia mashuhuri duniani Mohammed Ali yamefanyika katika jimbo la Kentucky, Marekani. Ali alifariki wiki iliyopita akiwa na umri wa miaka 74.  Maelfu ya watu, wakiwemo Waislamu kutoka maeneo mengi duniani, wamehudhuria swala hiyo katika ukumbi wa Freedom Hall, mjini Louisville.  Swala hiyo inapeperushwa moja kwa moja kupitia runinga na Waislamu wengi duniani wanatumai kwamba itaashiria mchango mzuri kwa dini ya Kiislamu nchini Marekani. Muhammad Ali alisilimu akiwa kijana. Alikuwa kwanza mwanachama wa madhehebu ya Nation of Islam, kundi lililotetea haki za watu weusi, lakini baadaye akakumbatia imani ya kawaida ya Kiislamu. Mazishi yake yatafanyika leo Ijumaa <a href='http://kwanza.co.tz/login/www/delivery/ck.php?n=a397efbc&cb=INSERT_RANDOM_NUMBER_HERE' target='_blank'><img src='http://kwanza.co.tz/login/www/delivery/avw.php?zone

Aliyemtukana Rais Magufuli Achangiwa Pesa

Image
VIJANA, wadau na wanaharakati wamefungua vikundi vya mtandao wa kijamii kwa ajili ya kuchanga fedha za kumsaidia kijana wa Arusha aliyepatikana na hatia ya kumtukana Rais na kuhukumiwa faini ya Sh7 milioni au kifungo. Kijana huyo, Isaack Habakuki wa Arusha alipatikana na hatia ya kumtukana Rais kwa kutumia ukurasa wake wa facebook na ametakiwa kulipa fedha hizo kwa awamu mbili na kuzikamilisha ifikapo Julai 7 au kwenda jela miaka mitatu. Diwani wa Kata ya Levolosi jijini Arusha (Chadema), Ephata Nanyaro ambaye anaratibu michango hiyo kwa mkoa wa Arusha, alisema mpaka sasa wameshakusanya Sh 800,000/- ambazo walizipata kwa njia ya kutuma kwa simu. Alisema wanatarajia kupata Sh1.7 milioni kutoka mikoa yote. “Tumesikia familia yake imeweza kutoa 3.5 millioni pekee, sisi tumejitolea kumsaidia ili afikishe 7 millioni kabla ya tarehe 7 mwezi julai,” alisema. 27

Chadema Wajifungia Kujadili hatua za kuchukua Dhidi ya Jeshi la Polisi Lililopiga Marufuku Maandamano na Mikutano

Image
Viongozi wa Chadema, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Vincent Mashinji jana walijifungia kutwa nzima kujadili hatua za kuchukua dhidi ya kitendo cha Jeshi la Polisi kuzuia maandamano na mikutano ya chama hicho ya kisiasa. Tangu asubuhi jana, viongozi hao walikuwa na kikao katika ukumbi wa Mandela, hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza na wakati wa mapumziko mafupi saa kumi jioni, Mbowe alisema chama hicho kitatoa kauli rasmi leo baada ya kikao kingine kilichotarajiwa kufanyika jana usiku. “Tutatoa kauli rasmi kesho (leo), baada ya vikao. Ninachoweza kuthibitisha ni kwamba tunaendelea kushauriana njia sahihi ya kuchukua,” alisema Mbowe. Juni 7, mwaka huu polisi ilitangaza kupiga marufuku kwa muda usiojulikana maandamano na mikutano yote ya kisiasa kwa kile kilichodaiwa ni taarifa za kiintelijensia za kuwapo tishio la kiusalama na kuwa wanakwenda kushawishi wananchi kuipinga Serikali. Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Zanzibar), Salum Mwalimu alis

Wasichana 500 wa Tanzania wanatumika Asia

Image
 Wasichana 500 wa Tanzania wanatumika Asia Serikali ya Tanzania imesema zaidi ya wasichana 500 raia wa nchi hiyo wanatumikishwa katika kazi hatari zikiwemo za ukahaba katika nchi za Asia na Uarabuni. Taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya Tanzania imesema imepata taarifa kuwa kuna mtandao unaowasafirisha wasichana katika nchi hizo kwa madai ya kufanya kazi za ndani lakini baadae hutumikishwa kwenye biashara ya ngono. Taarifa zinasema baadhi ya wasichana hao wemekimbilia kwenye ubalozi wa nchi hiyo ili kuomba kurudishwa nyumbani Mindi Kasiga ni Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya Tanzania ambaye anasema '' Mtandao huo unachofanya ni pamoja na kuwatafuta wasichana wenye umri kati ya miaka 18 na 24 na hata chini ya umri huo na kuwalaghai kuwa kuna fursa za ajira katika mahoteli, migahawa, maduka makubwa au kazi za nyumbani nchi za nje na kwamba watawasaidia wasichana hao kupata kazi hizo pamoja na kuwawezesha kupata vyeti vya kusafiria VISA na tiketi za ndege kwa

Muhammad Ali Kuzikwa Kishujaa Leo

Image
Muhammad Ali LOUISVILLE, Marekani GWIJI wa ndondi duniani, Muhammad Ali, anatarajiwa kuingizwa kwenye nyumba yake ya milele kwa heshima kubwa leo Ijumaa baada ya sara maalum ya Kiislam huko Louisville, Kentucky, Marekani. Ratiba ya sara za mazishi, ilianza juzi Jumatano na jana zaidi ya watu 14,000 kuzikwa kishujaa leo waliungana kuomboleza kwa sala katika ibada iliyorushwa moja kwa moja kwenye televisheni. Ali, alifariki dunia Ijumaa iliyopita akiwa na umri wa miaka 74 baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na ugonjwa wa Parkinson ambao unashambulia mfumo wa seli. Mazishi yake leo yanatarajiwa kushirikisha wawakilishi kutoka dini mbalimbali wakiwemo Wayahudi na Wakristo. Ali, alianza kupanga jinsi mazishi yake yatakavyokuwa mwaka mmoja uliopita na akasisitiza yawe huru kwa kila mmoja anayetaka kuhudhuria, afanye hivyo bure, familia imethibitisha. Ali ameacha mke na watoto tisa.