Posts

Showing posts from September 22, 2015

Sumaye: CCM Kama Kuna Hirizi Zenu Ikulu, Mzitoe Mapema

Image
Aliyewahi kuwa waziri mkuu wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Fredrick Sumaye, ametupa ‘Dongo’ kwa mahasimu wao kisiasa CCM, waanze kufungasha ‘virago’ mapema kwa kuwa mwaka huu ni wa UKAWA. Akizungumza jana na mamia ya wananchi Dar es salaam, Sumaye amedai kwa miaka mingi CCM imekuwa ikiahidi ahadi bila utekelezaji, hivyo amewataka wananchi kumpigia kura nyingi mgombea wa CHADEMA/UKAWA Edward Lowassa. “Niwaambie kabisa waanze kuondoka kuiachia Ikulu mapema, kama kuna hirizi zao waziondoe mapema waiache Ikulu ikiwa safi”. SOURCE: Times fm Radio.

KILIO KIKUBWA: CCM YAPATA PIGO ZITO BAADA YA MGOMBEA WAO KUFARIKI DUNIA, HALI NI TETE KWA WAGOMBEA

Image
Mgombea udiwani kata ya Muleba Wilaya ya Muleba Kusini, kwa tiketi ya CCM, Osward Rwakabwa amefariki dunia kwa ajali ya pikipiki. Osward ni mgombea wa tatu udiwani kwa tiketi ya CCM kata ya Muleba kufa akiwa katika harakati za kampeni za Uchaguzi Mkuu kwani wa kwanza alikufa mwaka 2005, 2010 na mwaka huu 2015. Osward alifariki katika hospitali ya serikali ya Kaigala alikopelekwa mara baada ya ajali hiyo iliyotokea jana jioni katika maeneo ya Tanesco akaribu na viwanja vya michezo vya Zimbiile Wilaya ya Muleba Kusini. Walioshuhudia ajali hiyo walisema marehemu ambaye alikuwa akiendesha pikipiki aligongana na pikipiki nyingine ambayo mmiliki wake alikimbia baada ya ajali hiyo. Kwa mujibu wa mashuhuda hao, Osward alikuwa akivuja damu kwenye pua na kwenye masikio mara baada ya ajali hiyo lakini alifariki katika hospitali hiyo. Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli alikwenda moja kwa moja nyumbani kwa marehemu Muleba kuhani msiba kabla ya kuanza mkutano wak...

MAGAZETI YA LEO JUAMANNE TAREHE 22.09.2015

Image