ORODHA YA WATUMISHI HEWA NCHI NZIMA YATUA SERIKALINI
HATIMAYE wakuu wa Mikoa yote nchini wametii agizo la Rais John Magufuli lilokuwa linawataka wasilishe ripoti ya idadi ya watumishi hewa kwenye mikoa husika. Wakuu hao wa mikoa wapya wamewasilisha ripoti za watumishi hao leo Jijini Dar es Salaam,Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Georgy Simbachawene ili kuchukuliwa hatua za kisheria kwa watumishi waliohusika katika kashfa hizo, Mkoa wa Dar Es Salaam . Akiwasilisha ripoti ya watumishi hewa.Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema katika mkoa wake baada ya kufanya uchunguzi kwa kushirikiana na kamati mbali mbali wamebaini kuwepo kwa watumishi hewa 73 ambao watumishi hao hewa wamepelekea serikali kupotea pesa zaidi ya Milioni 316 kwa mwaka mmoja. “Katika mkoa huu tumepata watumioshi hewa 73,ila wengi watahoji mkoa huu mkubwa kwanini unakuwa na watumishi hewa wachache,nakata kukwambia Waziri, bado tunaendelea na uchunguzi wa kina”amesema Makonda . Mkoa wa Arusha.