Posts

Showing posts from February 8, 2017

RC MAKONDA ATAJA LISTI NYINGINE YA MAJINA 65 YA WANAOHUSIKA NA DAWA ZA KULEVYA

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametaja majina ya watuhumiwa wengine 65 wa madawa ya kulevya, wakiwemo Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Jimbo la Hai, Freeman Elikael Mbowe, Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, Askofu Josephat Gwajima na Mbunge Mstaafu wa Kinondoni, Idd Azzan. Makonda amesema hii ni awamu ya pili ya oparesheni ya kusaka watuhumiwa wa mtandao wa biashara haramu ya madawa ya kulevya, ambapo amesema awamu hii itakuwa ngumu ikilinganishwa na ile ya kwanza iliyohusisha polisi na wasanii kukamatwa. Makonda amewataka watu wote 65 waliotajwa, kuhakikisha wanaripoti kwenye Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam (Sentro) siku ya Ijumaa saa 5 asubuhi kwa mahojiano zaidi. Akizungumza na wanahabari ofisini kwake, Makonda amesema kuwa, waliokamatwa awali ndiyo waliofanikisha kupatikana kwa orodha hiyo mpya.

WIZARA YA HABARI YAZINDUA PROGRAMU YA WADAU TUZUNGUMZE

Image
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza na waandishi wa habari (hawapo Pichani) leo Februari 07, 2017 Jijini Dar es Salaam kuhusu mkakati wa Wizara kuanza kuzungumza na wadau katika sekta zinazosimamiwa na Wizara yake. Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (hayupo pichani) akizungumza leo Februari 07,2017 Jijini Dar es Salaa kuhusu mkakati wa Wizara kuanza kuzungumza na wadau wa sekta zinazosimamiwa na Wizara yake. Picha na Raymond Mushumbusi Na: Genofeva Matemu  Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imebuni na kutanganza Programu ya kushirikisha wadau inayoitwa wadau tuzungumze itakayosaidia wizara kupata vionjo, maoni, mawazo na fikra za wadau katika kuhakikisha kwamba Wizara inafanya kama wadau wake wanavyotegemea. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof.

MTOTO WA DARASA LA NNE AFANYIWA UKATILI KWA KUCHOMWA MOTO MIKONO JIJINI DAR ES SALAAM

Image
Bi.Tatu Rashid mkazi wa Kivule jijini Dar es Salaam amemfanyia ukatili mtoto wake wa kumzaa kwa kumfunga mikono yake miwili,kisha kumuwekea mifuko ya plastiki na kumchoma moto baada ya mtoto huyo kudaiwa kuchukua shilingi 1000. Tukio hilo la kikatili alilofanyiwa mwanafunzi wa darasa la nne jina linahifadhiwa, limetokea jana eneo la Kivule jijini Dar es Salaam,ambapo ITV baada ya kubaini ukatili huo ilifuatilia sakata hilo na kukuta suala hilo likiwa limefikishwa katika ofisi ya serikali ya mtaa wa huo, ambapo mtoto huyo ambaye jina lake limehifadhiwa ambaye ni mwanafunzi wa darasa la nne ameeleza kwamba licha ya licha kumuomba msamaha mama yake mzazi kwa kuchukua shilingi 600 bila kumuomba lakini mama yake hakumuhurumia na badala yake alilazimisha kuwa kachukua shilingi 1000 jambo ambalo limemuhuzunisha baba mzazi wa mtoto ambaye hakuwepo nyumbani wakati wa tukio. Majirani wa familia hiyo wamesema mama huyo baada ya kuona mtoto wake atagundulika kach