Posts

Showing posts from March 30, 2017

BREAKING: Mahakama kuu yaamuru Mbunge wa Chadema aliyefungwa miezi 6 jela aachiwe huru

Image
Mahakama Kuu Dar es Salaam imetengua hukumu iliyotolewa na Mahakama ya W/Kilombero dhidi ya Mbunge Peter Lijualikali, amekutwa hana hatia. Mahakama Kuu kanda ya Dar ES Salaam imetengua hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Wilaya Kilombero dhidi ya Mbunge Peter Lijualikali baada ya kukubaliana na warufani kwamba hati ya mashtaka iliyomtia hatiani ilikuwa na upungufu. Uamuzi huo umetolewa leo mbele ya Jaji Ama- Isaria Munisi baada ya kupitia sababu za kupinga mbunge huyo kutiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miezi sita jela. Peter aliwakilishwa mahakamani na Wakili Tundu Lissu na Fred Kiwelo wakati Jamhuri ilikuwa ikiwakikishwa na Wakili wa Serikali, Faraja Nchimbi. Mshtakiwa mwingine aliyehukumiwa kifungo cha nje, Stephani Mgatta adhabu yake pia imetenguliwa. January 2017, Mahakama ya wilaya ya Kilombero ilimuhukumu kwenda jela miezi sita Mbunge wa jimbo la Kilombero, Peter Lijualikali (30) kwa kosa la kufanya fujo na kusababisha taharuki kati

Dakika 180 za Makonda Bungeni zilikuwa hivi...

Image
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda jana alihojiwa kwa saa tatu mfululizo na Kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge kwa tuhuma za kuingilia haki, uhuru na madaraka ya chombo hicho cha kutunga sheria. Makonda aliwasili Bungeni Dodoma majira ya saa nne asubuhi kuitikia wito wa Kamati hiyo uliotokana na Azimio la Bunge lililotolewa Februari 8 na kuhojiwa na kamati hiyo kwa muda wa saa tatu kuhusu tuhuma zinazomkabili. Katika kikao hicho, Bunge liliamua Makonda aitwe kujieleza kwenye Kamati ya Bunge ya Haki, Kinga na Madaraka kwa tuhuma za kukashfu chombo hicho.Sambamba na uamuzi huo, pia Bunge liliagiza mbunge yeyote ambaye kwa namna yoyote anadhani amekashfiwa na Makonda, awasilishe malalamiko yake kwa Spika ili hatua zaidi zichukuliwe. Hatua ya kutaka Makonda aitwe mbele ya kamati hiyo, ilitokana na mwongozo uliotolewa na Mbunge wa Mkuranga(CCM), Abdallah Ulega, kwa Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge, aliyedai mkuu huyo wa mkoa

KIJANA WA KITANZNAIA ANAYEISHI UJERUMANI AJA NCHINI KUTOA MAFUNZO YA KUCHEZA

Image
Mtanzania Emanuel Houston akizungumza na waandushi wa habari kuhusiana na mafunzo ya kucheza yatakayoendeshwa nae hapo kesho chini ya Unleashed Academy, kushoto ni msanii na mratibu wa mafunzo hayo Bernad Paul 'Ben Pol' na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Unleashed  Academy Halila Mbowe. Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii. Watanzania wenye vipaji wametakiwa kutumia fursa mbalimbali zinazojitokeza na wamewataka wajitokeze kwa wingi katika mafunzo ya kucheza yatakayoendeshwa na Mtanzania Emanuel Houston anayeishi Nchini Ujerumani.Emanuel ameambatana na baba yake Luis Houston ambao wote wanaishi nchini Ujeruami na wataendesha mafunzo hayo kupitia taasisi ya Unleashead Academy iliyo chini ya Halila Mbowe.Akizungumza na waandishi wa habari, Emanuel amesema kuwa anafurahi kuja kuwafundisha vijana wa kitanzania namna ya kucheza na watapata fursa ya kumuuliza kitu chochote.Emanuel amesema kuwa, kuja kwake nchini Tanzania anategemea kuona vijana wengi kuja kujifunza