Posts

Showing posts from May 1, 2017

KAJALA MASANJA AIBUKA TENA,SASA AMWANIKA MWANAUME WA KUMUOA

Image
MUIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja, amefunguka kuwa, endapo ataolewa tena, basi kigezo cha kwanza cha huyo mtarajiwa wake kitakuwa ni kudekezwa. Kajala ambaye aliolewa kisha ndoa yake kupata matatizo na mumewe kufungwa gerezani na hivi karibuni kuachiwa, alisema endapo itatokea ameolewa kwa mara nyingine basi kigezo cha huyo mwanaume ni lazima awe anayejua kudekeza. “Nampenda mwanaume mwenye mapenzi ya kweli lakini zaidi ya yote mimi napenda kudekezwa hivyo mwanaume atakayenioa lazima awe na sifa hizo vinginevyo atanisikia kwenye bomba,” alisema Kajala huku akiomba asimzungumzie mumewe ambaye ametoka gerezani hivi karibuni.

Lissu akomalia vyeti vya Bashite kortini

Image
WAWKILI Tundu Lissu na wenzake wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS) wamelikomalia vilivyo sakata maarufu la Bashite linalohusiana na tuhuma za kughushi vyeti vya kielimu linalomkabili mmoja wa wakuu wa mikoa kwa kulifikisha kortini ili lipatiwe ufumbuzi. Aidha, Lissu na wenzake hao wamedhamiria kuona kuwa kigogo huyo anayetuhumiwa kuliacha jina lake halisi la Daudi Albert Bashite kutokana na matokeo mabovu ya sekondari na kutumia jina la mtu mwingine, achukuliwe hatua za kisheria ikiwamo kufungwa jela kwa kosa la kughushi ikiwa itathibitika kuwa ana hatia. Akizungumza jana na waandishi wa habari mjini Dodoma jana, Lissu ambaye ni Rais wa TLS, alisema uamuzi huo wa kulifikisha mahakamani suala la Bashite umetokana na maazimio ya baraza la uongozi la chama hicho, lengo likiwa ni kulinda utawala wa sheria na uwajibikaji nchini. Tofauti na matarajio ya baadhi ya watu, sakata hilo la Bashite halikupatiwa jibu kutokana na ripoti ya uhakiki wa vyeti vy

Tujikumbushe :Hotuba ya Mwalimu Julius K. Nyerere Aliyitoa kwwenye Mei Mosi 1995

Image
Mwalimu Nyerere alialikwa kuwa Mgeni Rasmi kwenye kilele cha Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani iliyofanyika kitaifaUwanja wa Sokoine Mjini Mbeya Mei 1, 1995. Katika hotuba yake, Mwalimu alielezea historia ya Vyama vya Wafanyakazi duniani. Aidha alitumia fursa hiyo kutoa maoni yake kuhusu hali ya kisiasa na kiuchumi nchini pamoja na ushauri kuhusu mambo ambayo wananchi wanapaswa kuzingatia wakati wa Uchaguzi Mkuu mwezi wa Oktoba mwaka ule. Hasa sifa za wagombea nafasi za uongozi kuwa ni pamoja na kila mmoja kujiuliza ataifanyia nini nchi yake baada ya kuchaguliwa na anakwenda kufanya nini Ikulu? Ifuatayo ni hotuba ya Mwalimu. Ni muhimu kukumbuka kuwa hotuba hii imefuata mlolongo wa mazungumzo ambayo Baba wa Taifa alikuwa nayo kwa wananchi katika maeneo mbalimbali ambapo alikuwa anajaribu kuamsha dhamira ya viongozi wetu wa wakati ule. Hotuba hii ni miongoni mwa hotuba ambazo ukweli wa hoja zake ni hazina kubwa kwa vizazi vijavyo vya Watanzania. Mwenyekiti wa OTTU, Vi

Hiki ni kizaazaa kingine fao la kujitoa

Image
NI kizazaa kingine! Baraza la Uongozi la Chama cha Mawakili wa Tanganyika(TLS), limeazimia kushirikiana na wadau kwenda mahakamani kuhoji kuhusu utata juu ya fao la kujitoa uanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii. Hivi karibuni wakati serikali ikiwa katika maandalizi ya kuliondoa fao hilo, kulizuka taharuki kwa baadhi ya wafanyakazi walio wanachama wa mifuko hiyo. Ilielezwa kuwa fao la kujitoa likiondolewa litaletwa fao la kutokuwa na ajira. Katika mapendekezo hayo mapya, inaelezwa kuwa mfanyakazi ambaye amechangia zaidi ya miezi 18, atalipwa asilimia 30 ya mshahara wake wa mwisho baada ya kupoteza ajira. Mbali na hilo, pia atalipwa kwa miezi sita mfululizo, kisha malipo hayo yatasitishwa. Anayestahili malipo hayo ni yule ambaye hakuacha kazi kwa hiari yake (resignation). Inaelezwa katika mapendekezo hayo ya awali kuwa baada ya miaka mitatu tangu kusitishwa kwa fao la kujitoa, mfanyakazi atakayekuwa hajapata ajira ataruhusiwa kuhamisha michango yake kutoka

Magufuli aombewa madaraka yasimlevye

Image
RAIS John Magufuli amewaomba  viongozi wa dini nchini wakiwamo maaskofu baada ya kuwataka wamwombee ili kazi yake ya urais isimpe kiburi bali aendelee kuwa mtumishi mwema wa watu. Rais Magufuli alitoa ombi hilo kwa nyakati tofauti jana wakati aliposhiriki ibada ya Jumapili kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Moshi Mjini na Kanisa Kuu la Kiaskofu la Parokia ya Kristo Mfalme (la katoliki), pia la Moshi Mjini, mkoani Kilimanjaro. Magufuli aliomba maaskofu na viongozi wengine wa dini wamuombee wakati akiwa katika kanisa la Usharika wa Moshi, kwenye ibada iliyoongozwa na Mkuu wa Kanisa la KKKT Tanzania, Askofu Dk. Fedrick Shoo na baadaye katika Kanisa la Kristo Mfalme ambako ibada iliongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Moshi, Mhashamu Isaac Amani. Awali, akiwa katika kanisa la KKKT, Askofu Shoo alimuomba Rais Magufuli kujitenga na washauri wanaojikomba na badala yake apokee ushauri unaotolewa na washauri wema na wenye nia njem