Shule iliyotokea mlipuko wa bomu yafungwa
Uongozi wa Shule ya Msingi Kihinga umaamua kuifunga kwa muda shule hiyo kwa lengo la kuwajenga kisaikolojia wanafunzi wake baada ya wenzao kupoteza maisha kutokana na mlipuko wa bomu. Akizungumza Mwananchi leo Novemba 10 ,Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Aidan Makobero amesema shule hiyo imefungwa kimasomo hadi Jumatatu ili wanafunzi waweze kupata malezi ya kisaikolojia Aidha amesema kwa shule jirani ya Nyarukubala iliyo karibu na mpakani na Burundi mahudhurio yamepungua kutoka wanafunzi 700 na kufikia 100 leo Novemba 10 “Hata shule nyingine ya Nyarulama nayo wanafunzi wake wamepungua baada ya tukio la shuleni kwangu na kusalia majumbani wakiogopa kwenda shule wakidai nao wanaweza kukumbwa na tukio kama la shule jirani’’ amesema Makobero Pia majeruhi 33 kati ya 42 waliojeruhiwa kwa bomu wameruhusiwa na kurejea makwao baada ya afya zao kuimarika Mganga wa hospitali ya misheni ya R...