Posts

Showing posts from March 9, 2016

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AMLAKI RAIS WA VIETNAM MHE. TRUONG TANG SANG IKULU

Image
Rais wa Vietnam Mhe. Truong Tang Sang akiwa pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia wananchi na wafanyakazi wa Ikulu mara baada ya kuwasili. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais wa Vietnam Mhe. Truong Tang Sang wakati walipokuwa wanazungumza Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza Mazungumzo Rasmi kati ya ujumbe wa Tanzania na Ujumbe wa Rais wa Vietnam Mhe. Truong Tang Sang Ikulu jijini Dar es Salaam Rais wa Vietnam Mhe. Truong Tang Sang akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuzungumza na wanahabari hawapo pichani Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari hawapo pichani kuhusu mazungumzo yao na Rais wa Vietnam...

MAMA JANETH MAGUFULI AMKARIBISHA MKE WA RAIS WA VIETNAM, BI. MAI THI HANH OFISINI KWAKE.

Image
  Mke wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh (mwenye gauni jekundu) akisalimiana na akina mama waliompokea mara alipotembelea katika ofisi za mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Janeth Magufuli 9 Machi, Ikulu Jijini Dar es Salaam. Mke wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh (mwenye gauni jekundu) akisalimiana na wacheza ngoma mara alipotembelea katika ofisi za mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Janeth Magufuli 9 Machi, Ikulu Jijini Dar es Salaam. Mke wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh akisaini kitabu cha wageni mara alipowasili katika ofisi za mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Janeth Magufuli (kulia) 9 Machi, Ikulu Jijini Dar es Salaam. Mke wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh (kushoto) akifurahia zawadi ya kinyago cha kuchonga alichokabidhiwa na mwenyeji wake mama Janeth Magufuli kama zawadi 9 Machi, 2016 katika ofisi za Mke wa Rais Jijini Dar es Salaam. Mke wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Th...

RAIS MAGUFULI AWATAKA WATANZANIA KUJIFUNZA KUTOKA KWA VIETNAM

Image
Na. Lilian Lundo - Maelezo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewataka watanzania kujifunza kutoka kwa Vietnam namna ambavyo wameweza kupambana na umaskini kwa muda mfupi. Mhe. Rais aliyasema hayo leo Ikulu katika ziara ya Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam Mhe. Truong Tan Sang baada ya kusaini mkataba wa kukuza uhusiano baina ya Tanzania na Vietnam. “Tanzania tunatakiwa tujifunze mambo mengi kutoka kwa wenzetu Vietnam ambao walipata uhuru mwaka 1945 wakaingia kwenye mapigano mpaka mwaka 1976. Wakati huo pato la muvietnam mmoja lilikuwa dola 100 lakini leo ni dola 2000 na wamepunguza umaskini kwa asilimia 50 kuifanya nchi hiyo kuwa ya kipato cha kati,” alisema Mhe. Rais Mhe. Rais Magufuli aliongezea kuwa, mwaka 1976 Vietnam ilichukua mbegu ya korosho kutoka Tanzania na kwenda kulima kwao, zao hilo limekuwa likifanya vizuri kwa nchi yao na wanaongoza kwa kulima korosho Duniani. Kwa upande wa Tanzania zao hilo lime...

RAIS DKT. MAGUFULI AMTEMBELEA NA KUMJULIA HALI MAALIMU SEIF SHARIF HAMAD.

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF ambaye pia ni Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad jijini Dar es Salaam. Maalim Seif aliruhusiwa kutoka hospitalini jana na hali yake inaendelea vizuri.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF ambaye pia ni Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad jijini Dar es Salaam. Maalim Seif amemshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa kumjulia hali  na kusema kuwa hali yake ya kiafya inaimarika siku baada ya siku. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF ambaye pia ni Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad jijini Dar es Salaam mara baada ya kumjulia hali jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS TUONG WA VIETNAM LEO

Image
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akimkaribisha Rais wa Vietnam Truong Tan Sang, kwa ajili ya mazungumzo ya pamoja na viongozi wengine katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Rais huyo yupo katika ziara ya kikazi nchini.  Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiwa katika mazungumzo ya pamoja na viongozi wengine na Rais wa Vietnam Truong Tan Sang na ujumbe wake, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Rais huyo yupo katika ziara ya kikazi nchini. Wapili kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Zakia Meghji na Waziri Mahiga.   Rais Truong wa Vietnam akimsifia jambo, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akati akimuaga baada ya mazungumzo yake na Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete (kulia)   Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiwa katika mazungumzo ya pamoja na viongozi wengine na Rais ...

MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI TUKIO LA KIHISTORIA LA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI.

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitoa risala yake ya ufunguzi kwenye Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani jijini Dar es salaam jana jioni katika tukio lililoandaliwa na Kazi Services Ltd kwa kushirikiana na Chama cha Waajiri nchini (ATE) na kudhaminiwa na mdhamini Mkuu Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). Balozi Dk Asharose Mtengeti Migiro akitoa ushuhuda wake wa namna alivyoweza kufanikiwa katika maisha pamoja na vikwazo vingi kwenye mfumo dume, kwenye Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani jijini Dar es salaam jana jioni katika tukio lililoandaliwa na Kazi Services Ltd kwa kushirikiana na Chama cha Waajiri nchini (ATE) na kudhaminiwa na mdhamini Mkuu Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na wadhamini wakuu wa tukio hilo la kihistoria kupata kutokea kwa kina mama Shirika la Nyu...