Posts

Showing posts from August 29, 2013

WAASI WA M23 WAMUUA MWANAJESHI WETU WA JWTZ HUKO KONGO

Image
TAARIFA KUHUSU TUKIO LA KUFARIKI KWA AFISA WA JWTZ KATIKA JUKUMU LA KULINDA AMANI - DRC, GOMA 1. Kama mnavyofahamu, JWTZ linashiriki katika operesheni za Umoja wa Mataifa huko Goma DRC. Kikosi chetu kimeendelea kutekeleza majukumu yake ya kulinda amani kama kinavyopangiwa na Jeshi la Umoja wa Mataifa nchini DRC lijulikanalo kama MONUSCO. 2. Tarehe 28 Agosti 2013 wanajeshi wetu wakiwa katika eneo lao la Ulinzi waliangukiwa na bomu katika eneo hilo na kusababisha majeruhi. Wakati wanapelekwa hospitali kwa matibabu, kwa bahati mbaya mwanajeshi wetu mmoja, Meja Khatibu Mshindo alifariki dunia. Majeruhi wengine wanaendelea na matibabu, na hali zao zinaendelea vizuri. 3. MONUSCO inaandaa utaratibu wa kuleta mwili wa marehemu. Imetolewa na: Kurugenzi ya Habari na Uhusiano Makao Makuu ya Jeshi. Dar es Salaam.

MFALME QABOOS ATOA MSAADA KWA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

Image
Na Kassim Ali na Amina Abeid (ZJMMC) Sultan Qaboos wa Oman ametoa msaada wa Riali milioni tatu na laki moja za nchi hiyo  kwa ajili ya  ujenzi wa Msikiti mkubwa  utakaojengwa katika  eneo la Chuo cha Kiislamu Mazizini nje kidogo ya mji wa Zanzibar.  Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Mazizini,  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Ali Juma Shamhuna amesema ujenzi  wa msikiti huo unatarajiwa kuanza  wakati wowote baada ya kutiwa saini makubaliano ya msingi kati ya Zanzibar na Oman. Amesema msikiti huo, pamoja na shughuli za ibada, pia  utakuwa  ni chimbuko la kuanzishwa Chuo Kikuu cha Kiislamu Zanzibar na kufanikisha azma ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar marehemu Abeid Amani karume aliependekeza kujengwa Chuo Kikuu cha Kiislamu katika eneo hilo alipokifungua chuo hicho. “Maandaliz yote ya kujengwa msikiti huu yamekamilika na utakuwa ...

RAY C AOKOKA RASIMI...HIZI NI PICHA ZAKE AKIBATIZWA

Image
  Yule dada yetu msanii maarufu wa nyimbo za bongo fleva  leo hii amewaka bayana ya kuwa yeye na shetani sasa ni paka na panya. Ray C amethibitisha hayo katika post zake za instagram. 

WAZIRI FENELLA AKUTANA NA BONDIA FRANCOIS BOTHA (WHITE BUFFALO)

Image
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara akielezea kufurahiswa kwake na ukuaji wa mchezo wa ngumi hapa nchini alipokutana na  Bondia maarufu duniani na aliyewahi kuwa bingwa wa dunia mara mbili  Francois Botha (White Buffalo) kushoto jana jijini Dar es Salaa. Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara akiwa na  Bingwa wa duni mara mbili wa mchezo wa ngumi Bondia Francois Botha (White Buffalo)  wakipiga picha baada ya kukabidhiwa zawadi ya picha ya bondia huyo ikionyesha enzi za ujana wake jana jijini Dar es Salaam. Botha yupo nchini kufuatia kuwepo kwa pambano la ngumi la dunia litakalofanyika kesho huku likiwakutanisha mabondia Francis Cheka wa Tanzania na Phill William wa Marekani. Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt fenella Mukangara na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo waliokaa wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Wizara na wageni walioambatana ...

"FAMILIA IMENITENGA BAADA YA KUOA ALBINO'...MUME

Image
KIJANA aitwaye Priscus Mushi, mkazi wa Mbezi jijini Dar ambaye ni muumini wa Kanisa la Efatha linaloongozwa na Mchungaji Josephat Mwingira ameanika masikitiko yake baada ya kutengwa na baadhi ya ndugu kufuatia kuoa mlemavu wa ngozi ‘albino’ aitwaye Tumaini Murungu. Akizungumza katika Ukumbi wa Maji uliopo maeneo ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo sherehe za ndoa zilifanyika, Mushi alisema alipotangaza nia ya kumuoa Tumaini baadhi ya ndugu zake walimtenga lakini hakukata tamaa kwani aliendelea na taratibu za ndoa. “Nilimpenda sana Tumaini na niliamini ndiye mwanamke wa maisha yangu lakini nilipowaambia ndugu zangu kuwa nataka kumuoa, baadhi walinitenga kwa uamuzi wangu huo wa kumuoa Tumaini ambaye ni mlemavu wa ngozi eti nitakuwa nimeleta balaa nyumbani. “Nilimuomba Mungu anisaidie na nikaongea na waumini wenzangu ambao walikubali kunifanyia sherehe.  Nawashukuru sana wakwe zangu ambao walinipokea na kunipa ushirikiano katika kulitimiza tukio hili. ...

Edward Lowassa asherekea kutimiza Miaka 60!

Image
HONGERA SANA MHESHIMIWA LOWASSA. Mwalimu Alikuwa Mwalimu, Atabaki Kuwa Mwalimu... Hii ilikuwa 1967. wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya wakutana kutoa maoni ya rasimu ya Katiba Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro(katikati) akisisitiza jambo leo juu ya maoni ya wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kuhusu rasimu ya Katiba katika ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari –MAELEZO jijini Dares Salaam na kushoto wa kwanza ni Mkurugenzi wa Idara ya hiyo, Assah Mwambene WATU 13 WAFA NA 11 MAJERUHI AJALI MBAYA MKOANI SHINYANGA ...

VIDEO YA UCHI YA MRISHO NGASA AKIWA NA MDOGO WAKE FLORAH MBASHA GESTI YAVUJA

Image
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya soka, Taifa Stars na mchezaji wa Yanga, Mrisho Ngasa, ameingia kwenye scandal nzito baada ya mkanda wake wa ngono kuvuja mtandaoni.   Mkanda huo  unamuonesha mchezaji huyo akiwa kwenye ‘suti yake ya kuzaliwa’ pamoja na msichana wakivunja amri ya sita.   Huku kukisikika muziki wa aina mbalimbali ukiwemo wa reggae, wapenzi hao wanasikika wakizungumza na kucheka wakati wakiendelea na tendo hilo.   Video  imewekwa  hapo  c hini << BOFYA  HAPA  KUIONA  VIDEO>>

BASI LA HOOD LAUA MTU MMOJA NA KUJERUHI 15

Image
Mtu mmoja amefariki dunia na 15  wamejeruhiwa baada ya basi  la Kampuni ya Hood  likitokea kilombero kwenda jijini  Dar es salaam kumgonga  mtembea kwa miguu na kisha kuacha njia na kupinduka katika eneo la Kiembeni  Mikese Mkoani  Morogoro.    Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Morogoro  Bonifasi Mbao  akizungumza kwenye  eneo la tukio amesema chanzo cha ajali  hiyo ni mwendo kasi ambapo dereva wa basi  gari  ilimshinda na kugonga mtembea kwa miguu na kisha kupinduka ambapo  dereva wa basi amekimbia mara baada ya tukio la ajali...   Taarifa za  madaktari  katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro  zimeeleza  majeruhi wanaendelea na matibabu na mwili wa marehemu umehifahiwa katika chumba cha maiti hospitali ya mkoa wa morogoro . -ITV