Maneno ya Tundu Lissu juu ya ripoti ya pili ya kamati maalum ya uchunguzi wa madini
For the Record: What Goes Around Comes Around!!! Leo wapinzani wa Serikali ya Magufuli tumesemwa sana na kutishiwa kushughulikiwa bungeni na nje ya Bunge. Kwa sababu hiyo, naomba niweke rekodi ya masuala haya sawa sawa. Mwezi Machi '97 Bunge lilipitisha Sheria 2 kwa siku moja kwa kutumia Hati ya Dharura. 1) Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbali mbali za Fedha ya '97 ilifuta au kupunguza kodi nyingi kwa ajili ya makampuni ya kigeni ya madini. 2) Sheria ya Uwekezaji Tanzania '97 iliwapa wawekezaji wa kigeni ulinzi mkubwa na manufaa mengi kama vile kuondosha nje fedha na faida yote wanayopata kwa uwekezaji wao nchini. Mwaka '98 Bunge lilipitisha Sheria ya Madini '98 ambayo ilitamka kwamba mwenye milki ya madini na fedha yote itokanayo na mauzo ya madini ni mwenye leseni ya kuchimba madini hayo. Sheria hizo tatu nimeziita 'Utatu Usio Mtakatifu' (Unholy Trinity) katika maandiko yangu mbali mbali, na nimezichambua sana tangu mwaka ...