Dk Vincent Mashinji. KATIBU Mkuu wa Chadema , Dk Vincent Mashinji amesema polisi wamemhoji wakitaka kujua kuhusu kauli zake za watu wasiojulikana kama anaweza kuwatambua. “Watu wasiojulikana ambao tulikuwa tunawaongelea ni kwamba, imezoeleka kwa polisi kunapokuwa na tukio kubwa wanasema watu wasiojulikana, kwa hiyo lengo langu lilikuwa ni kuita wananchi kurudi kwenye Polisi Jamii ili kuondokana na hili la watu wasiojulikana,” alisema Dk Mashinji. Katibu mkuu huyo wa Chadema, leo Jumatatu ameamua kwenda kuripoti Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini hapa. Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Chadema, Tumaini Makene ilisema Dk Mashinji aliambatana na wasaidizi wake kutoka makao makuu ya chama hicho. “Katibu mkuu amewasili Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam, kuitikia wito wa Polisi uliotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, kuwa anatakiwa kufika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jina...