Posts

Showing posts from February 26, 2016

Taswira ya Msiba wa Mapili

Image
Waombolezaji wakiwa msibani. Mtangazaji na Mdau wa Muziki wa Dansi, Rajab Zomboko akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani). Msanii wa muziki, Mrisho Mpoto akitoa ratiba ya maziko. Muimbaji wa Twanga Pepeta, Luiza Mbutu akiwa na waombolezaji wengine. Aliyekuwa Mbunge wa Kinondoni, Iddi Azan akiwa msibani hapo. Mtangazaji wa Global TV Online, akimhoji Mkongwe King Kiki kuhusu marehemu. Mamia ya waombolezaji wamejitokeza mapema leo kumsindikiza Mkongwe wa Muziki wa Dansi na Mlezi wa Bendi ya Mjomba, Kassim Mapili baada ya kufariki ghafla akiwa nyumbani kwa mwanaye, Magomeni Mapipa jijini Dar es Salaam. Picha/ Chande Abdallah

AIBU M MPYA YA BOSI LADY.

Image
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mpenzi wake Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’. Stori: Mwandishi, Wetu, Ijumaa D ar es Salaam: Aibu yake! Kitendo cha mwandani wa Mwanamuziki wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kutupia mtandaoni picha ya nusu utupu akiwa amelala na jamaa huyo, kimetafsiriwa kuwa ni kulipa kisasi kwani miezi kadhaa iliyopita naye alimtundika akiwa anaoga bafuni. Mpenzi wa mwanamuziki wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’. Picha hiyo ya mapema wiki hii, inadaiwa Zari aliitupia kwenye akaunti yake ya Mtandao wa Instagram kisha kuitoa muda mfupi bila kujua imeshachukuliwa na wapenda ubuyu na kurushwa kwenye meza ya Ijumaa.   Zari The Boss Lady akiwa na Diamond Platinumz. DIAMOND FOFOFO Katika picha hiyo, Zari anaonekana ndiye aliyeipiga ikiwaonesha wakiwa wamelala kitandani huku Diamond akiwa fofofo bila kujua kilichoendelea. Picha hiyo iliibua g...

WAZIRI KITWANGA AKUTANA NA VIONGOZI WA NIDA, AWATAKA KUONGEZA KASI UANDAAJI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA

Image
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akizungumza na Watendaji Wakuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji wa kazi ndani ya Mamlaka hiyo na Wizara kiujumla. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Wa kwanza upande wa kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira akifuatiwa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Lilian Mapfa. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa NIDA, Dk. Modest Kipilimba. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akizungumza na Watendaji Wakuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji wa kazi ndani ya Mamlaka hiyo na Wizara kiujumla. Kikao hicho kilifanyika...

Kajala sasa ajis’tukia kuzeeka

Image
Na Imelda Mtema Staa wa Filamu Bongo, Kajala Masanja amesema kuwa mambo ya kimjini kama wafanyavyo mastaa wengine kwa sasa ameyapa mgongo kwa madai kuwa anaona anaelekea kuzeeka. Akizungumza na mwandishi wa habari hii hivi karibuni, Kajala alisema kila anapojiangalia anaona kabisa alivyokuwa zamani sivyo alivyo sasa hivyo ana kila sababu ya kubadilika. “Kiukweli najiona kabisa naelekea kuzeeka, ule usichana unapotea hivyo ni vyema sasa mambo mengine ya kimjini nikayapa kisogo. Kwenda klabu usiku nimepunguza na kuna siku nitaacha kabisa, nguo za ajabuajabu najifikiria mara mbilimbili,” alisema Kajala.

SERIKALI YAWAKUTANISHA VIJANA KUUNDA KANUNI ZA UENDESHAJI BARAZA LA VIJANA TAIFA.

Image
  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye ulemavu Bw. Eric Shitindi akizungumza na vijana (hawapo pichani) alipokuwa akifungua kikao cha wadau wa maendeleo ya vijana katika kuchangia uandaaji wa kanuni za uendeshaji wa Baraza la Vijana Taifa jana jijini Dar es Salaam.   Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi akizungumza wakati wa kikao cha wadau wa maendeleo ya vijana katika kuchangia uandaaji wa kanuni za uendeshaji wa Baraza la Vijana Taifa jana jijini Dar es Salaam.   Mwezeshaji Bw. Patrick Kipangula (aliyesimama) akitoa mada kwa wadau wa maendeleo ya vijana wakati wa kikao cha kuchangia uandaaji wa kanuni za uendeshaji wa Baraza la Vijana Taifa jana jijini Dar es Salaam.   Mjumbe    wa maendeleo ya vijana akichangia mada wakati wa kikao cha kuchangia uandaaji wa kanuni za uendeshaji wa Baraza la Vijana Taifa jana jijini Dar es Salaam.   Wawakilishi kutoka Mamlaka mbalimb...

Wasira: Nilianza kupigwa picha tangu natoka chooni, nahisi huyu katumwa

Image
Mwanasiasa mkongwe na Waziri wa zamani wa Chakula, Kilimo na Ushirika, Stephen Wasira ameeleza sababu zilimpelekea kugeuka mbongo na kutaka kumgonga na gari mwandishi wa habari aliyekuwa anampiga picha. Wasira ameeleza kuwa alipandishwa hasira na kitendo cha mpiga picha, Michael Samson kumpiga picha nyingi zisizo na idadi huku akimfuata kila anapoenda, punde tu alipotoka msalani. “Nilianza kupigwa picha wakati natoka chooni tukiwa pale Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza. Nikamuuliza yule kijana, ‘hizi picha zote unanipiga ni za nini?’ akananiambia ni za habari. Nikamuuliza picha zote hizo mia ni za habari? Yeye akaendelea tu kunipiga picha,” Wasira ananukuliwa na gazeti la Mwananchi. Wasira alikutana na tukio hilo katika jengo la Mahakama ya Biashara jijini Mwanza baada ya kutoka Mahakama Kuu ya Kanda ya Mwanza, alipokuwa akifuatilia rufaa yake ya kupinga matokeo ya ubunge wa jimbo la Bunda Mjini yaliyompa ushindi Ester Bulaya (Chadema). Mwanasiasa huyo mkongwe alija...

RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI AMLILIA MZEE KASSIM MAPILI

Image

MAWAZIRI WAPEWA MWISHO LEO KUJAZA TAMKO LA MALI NA MADENI, HATI YA UADILIFU

Image
  Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majliwa Majaliwa (kulia) akitoa taarifa mbele ya Waandishi wa Habari kuhusiana na misingi ya Fomu za Maadili ya Utumishi wa Umma kwa Viongozi wa Umma pamoja na kujaza fomu za tamko za rasilimali walizo nazo na za madeni waliyonayo sambamba na kutaja majina ya baadhi ya Mawaziri na Manaibu Waziri ambao bado mpaka sasa hawajarudisha fomu hizo kwa Kamishna. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki.   Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (hayupo pichani) wakati akitoa taarifa kuhusiana na misingi ya Fomu za Maadili ya Utumishi wa Umma kwa Viongozi wa Umma pamoja na kujaza fomu za tamko za rasilimali walizo nazo na za madeni waliyonayo sambamba na kutaja majina ya baadhi ya Mawaziri na Manaibu Waziri ambao bado mpaka sasa hawajarudisha fomu hizo kwa Kamishna. (PICHA ZOTE NA EBENED...

Vigogo Watatu Wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) Wafikishwa Mahakamani

Image
Vigogo watatu wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), akiwemo Mtendaji Mkuu wa mradi huo, Asteria Mlambo, wamepandishwa kizimbani, kwa tuhuma za kuisababishia serikali hasara ya Sh milioni 83.5. Mbali na Asteria, washitakiwa wengine wanaokabiliwa na mashitaka hayo ya uhujumu uchumi ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Evodius Katale, Mwanasheria Mkuu wa mradi huo, Francis Kugesha na Mkurugenzi wa kampuni ya Yukan, Yuda Mwakatobe. Walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam jana na kusomewa mashitaka matatu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage. Walisomewa mashitaka na wakili kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Jackline Nyantori akisaidiwa na Estazia Wilson na Stellah Mafuru. Nyantori alidai kati ya Septemba Mosi na Oktoba Mosi 2013, Kinondoni Dar es Salaam, Asteria, Katale na Kugesha wakiwa wafanyakazi wa mradi huo, walishindwa kutekeleza majukumu yao vizuri na kuisababishia serikali hasa...