Posts

Showing posts from February 13, 2018

Chama cha Wafanyakazi chapingana na Makonda

Image
Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (Talgwu) kimelaani kitendo kikichofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda cha kuwavua madaraka hadharani watumishi wa umma wakisema ni kitendo cha kinyama. Akizungumza leo Februari 13, 2018 wakati akitoa tamko la chama hicho, Katibu Mkuu, Rashid Mtima amesema chama hicho hakitetei watumishi waovu, bali taratibu zinatakiwa kufuatwa katika kuwawajibisha Februari 10, 2018  watumishi wa idara za ardhi wa manipaa za Ubungo na Ilala walivuliwa madaraka hadharani hali iliyosababisha mmoja wao, Paul Mbembela (Mkuu wa Idara ya Mipango Miji Ilala) kuzimia kwa muda. "Tunalaani, tunalaani, tunalaani sana kitendo kilichofanywa na Makonda. Sheria zinataka mtumishi anayekiuka kanuni na sheria za utumishi kushughulikiwa kwa siri hadi uamuzi wa mwisho utakapotolewa,” amesema. " Jambo baya zaidi tunalolaani hata mtumishi huyo alipozimia Makonda aliendelea kusema Dar es Salaam oyee, huu ni unyama.” Amesema kibin...

Diwani Mwingine Chadema Atimkia CCM

Image
DIWANI wa Kata ya Hayderer (Chadema) wilayani Mbulu mkoani Manyara, Justin Masuja amejiuzulu nafasi hiyo na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) jana Februari 12,2018 katika ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti. Katika mkutano wa hadhara, Mnyeti aliwaomba madiwani wa upinzani kuhamia chama tawala ili watekeleze Ilani ya CCM ambayo ndiyo ipo madarakani. Masuja alieleza kwamba amejiunga na CCM ikiwa ni hatua ya kuunga mkono jitihada za Rais John Magufuli katika kuwatumikia wananchi wa Tanzania.

Mwanamke abambwa na cocaine kwenye makalio

Image
Polisi nchini Ureno wamemkamata mwanamume mmoja kwenye uwanja wa ndege huko Lisbon, ambaye alikuwa amebeba kilo moja ya cocaine kwenye makalio bandia. Vyombo vya habari nchini humo vilisema kuwa raia huyo wa Brazil aliwasili kwa ndege kutoka mji wa Belém do Pará, kaskazini mwa Brazil. Haijulikani ni vipi polisi walifanikiwa kugundia hilo. Mwanamume mwingine ambaye anashukiwa kuwa angepokea dawa hizo alikamatwa kwenye kituo cha treni cha mji huo. Wanaume hao watakabiliwa na kesi ya ulanguzi wa madawa ya kulevya. Mwezi uliopita polisi nchini Ureno na Uhispania walikamata cocaine ndani ya mananasi yaliyokuwa yamessfirishwa kutoka Amerika ya Kusini.

KAULI YA KWANZA DIAMOND PLATINUMZ NA HAMISA BAADA YA KUTOKA MAHAKAMANI

Image
February 13, 2018 stori inayoshika headlines ni ya Kimahakama ambapo Nyota wa muziki wa Bongo fleva na President wa WCB, Diamond Platnumz na Mwanamitindo Hamisa Mobetto wamerudi tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kuweka rekodi baada ya usuluhishi wao kuhusu matunzo ya mtoto wao. “Hivyo tutaangalia jinsi ya kumtunza mtoto wetu ikiwezekana tunategemea baadaye anaweza kuwa kiongozi fulani . Nawashauri wababa kwamba wazazi wakike na kiume wajitahidi kuweka majivuno pembeni bila kumuathiri mtoto. Hivyo lazima kuweka majivuno pembeni kwani mwisho wa siku anayeathirika ni mtoto.” Diamond Platnumz <span data-mce-type="bookmark" style="display: inline-block; width: 0px; overflow: hidden; line-height: 0;" class="mce_SELRES_start"></span>

RAMAPHOSA AONGOZA JAHAZI KUMUNG’OA ZUMA MADARAKANI, AMPA SAA 48

Image
Rais Jacob Zuma. RAIS wa Afrika Kusini Jacob Zuma amepewa saa 48 kujiuzulu, wadhfa wake huo huku Kiongozi mpya wa ANC, Cyril Ramaphosa akiongoza shinikizo hilo la kumng’oa kiongozi huyo mkongwe barani Afrika.Kwa mujibu shirika la Utangazaji la Afrika Kusini -SABC- na vyanzo vingine vya habari, hatua hii inakuja baada ya mlolongo wa mazungumzo yaliyofanywa na chama tawala cha nchini humo ANC. Taarifa zinaeleza kuwa, ANC kilifanya mazungumzo marefu baadaye kuwatuma watu wawili nyumbani kwa Rais Zuma jijini Pretoria kwenda kumfikishia ujumbe wa chama ana kwa ana ya kwamba Zuma ajiuzulu mwenyewe au chama kimng’oe madarakani japo mpaka sasa haijulikani kwamba Rais Zuma alipokeaje ujumbe huo. Hatua hii ya ANC inaonekana ndio njia rahisi zaidi ya chama hicho kumng’oa rais Zuma madarakani badala ya kusubiri utaratibu wa bunge ambao ungeweza kuchukua muda mrefu na wenye madhara zaidi kwa Chama cha ANC. Rais Zuma ambaye anakabiliwa na mashtaka kadhaa ya rushwa, alishindwa...

ANGALIA BINTI WA MIAKA 11 AJIFUNGUA SIKU YA HARUSI YAKE,NI MAJANGAZI

Image
Binti wa miaka 11 wa nchini Bulgaria ambaye alijifungua mtoto wa kike siku ya harusi yake huku akiwa amevaa shela lake la harusi amesema hataki tena kuendelea na shule na anataka atumie muda mwingi kucheza na mtoto wake. Kordeza Zhelyazkova mwenye umri wa miaka 11 wa nchini Bulgaria alijifungua salama wiki iliyopita mtoto wa kike mwenye uzito wa kilo 2.4 ambaye alimpa jina la Violeta lakini alitoroka hospitali na mtoto wake usiku huo huo aliojifungua mtoto wake ili awahi kumalizia sherehe za harusi yake. Kordeza ambaye alikuwa ni mwanafunzi wa shule ya msingi, alisema kuwa alikutana na mumewe mpya mwenye umri wa miaka 19 Jeliazko Dimitrov kwenye viwanja vya michezo vya shule yake baada ya Jeliazko kumuokoa kutoka kwenye kipigo cha wahuni wa mitaani. Kordeza anadai alianza kufanya mapenzi na Jeliazko bila kutumia kondomu na anakiri alikuwa hajui kondomu ni kitu gani wakati huo. Kordeza alipata mimba ndani ya wiki moja baada ya kuanza kufanya mapenzi na mpenzi wa...