Mwanafunzi wa kike DSM ajinyonga kisa kupinga kusoma
Mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Tegeta jijini Dar es Salaam, Bertha Amir (14), pichani, amejinyonga hadi kufa akipinga kulazimishwa na mama yake mzazi kusoma. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura, alisema mwanafunzi huyo alijinyonga juzi saa 11:00 jioni, maeneo ya Tegeta Namanga, jijini Dar es Salaam. Alisema marehemu alikutwa amejinyonga chumbani kwa kutumia mtandio ulioning’inizwa juu ya dari. Kamanda Wambura alisema sababu za mwanafunzi huyo kujinyonga bado hazijafahamika, lakini akasema inasadikika kuwa wakati wa enzi za uhai wake, siku moja kabla ya kifo chake, alikuwa ameongea na mama yake, Angelina Maiko Mshami (30), ambaye alimtaka achukue fedha kwa ajili ya kujiandaa kwenda shule. Alisema mtoto huyo alimjibu mama yake kuwa hahitaji kusoma, bali anataka kufanya kazi. Kamanda alisema kuwa mwili wa mwanafunzi huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala kwa...