Binti Aliyedai Kutelekezwa na Lowassa Zengwe Jipya Laibuka!
U KISEMA unatafuta maisha usisahau kwamba kuna wakati nayo yanakutafuta ili mcheze ngoma moja; tuhuma za Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa kudaiwa kutelekeza mtoto zina funzo ndani yake. Siku chache baada ya msichana aitwaye Fatuma Lowassa kujitokeza ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na kutoa madai ya kutelekezwa na Lowassa na hatimaye ishu hiyo ‘kupotelea hewani’, Uwazi limenasa zegwe jipya. “Kama ni kujitokeza na madai hayo ya kutelekezwa na Lowassa hii si mara ya kwanza kwa msichana huyo, sikumbuki ni lini lakini miaka ya nyuma aliwahi kufanya hivyo. “Mi nawaamini mkifanya uchunguzi wenu mtapata jambo hili, kuna watu wanayo video ya mahojiano ya msichana huyo pamoja na mama yake wakilalamika kutelekezwa. “Mimi nimejaribu kuipata nimeshindwa ila nasikia inaandaliwa itolewe ili kufufua upya tuhuma,” chanzo makini kililidokeza Uwazi na kulifanya lipange kikosi kazi kwa lengo la kufuatilia uwepo wa video hiyo . Fat...