Chanzo Cha Maumivu Ya Tumbo Mara Kwa Mara!
Maumivu ya tumbo. MAUMIVU ya tumbo ni tatizo linaloweza kumpata mtu yeyote, mwanamke au mwanaume, mkubwa au mdogo. Maumivu haya husumbua kwani huwa hayaishi, yaani yanatulia kwa muda flani na kurudi tena, aina hii ya maumivu pia inaweza kuwa ya moja kwa moja, yaani hayatulii na wakati mwingine mgonjwa hupata nafuu kwa kujikunja au kushikilia tumbo. Maumivu yanaweza kuwa upande wa juu wa tumbo au upande wa chini na yanatulia kwa vipindi na kurudi yakiwa makali au madogo lakini hayaishi. JINSI TATIZO LINAVYOTOKEA Kama tulivyoona, humtokea yeyote mwanamke au mwanaume, utokeaji wake hutofautiana kwa jinsi. Kwa mwanaume vyanzo vya maumivu haya vinaweza kuwa hernia au ngiri au matatizo kwenye korodani, lakini kwa wote vyanzo vinaweza kuwa vidonda vya tumbo, matatizo ya mkojo, kidole tumbo, matatizo ya utumbo mkubwa, kukosa au kufunga kupata haja kubwa, gesi kujaa tumboni. Yapo mengine kama kuwa na mawe kwenye mfumo wa mkojo au kifuko cha nyongo, matatizo ya ini na mengi...