Posts

Showing posts from February 24, 2018
Image
 Msanii wa muziki Bongo,Ambwene Yesaya maarufu kama AY amefunga ndoa leo na mpenzi wake wa muda mrefu Remy. Shughuli za kufunga ndoa hiyo zimefanyika leo katika hotel ya Golden Tulip iliyopo jijini Dar Es Salaam na kuhudhuliwa na mastaa mablimbali kama vile:-Lady Jaydee, Mwana FA, Salama Jabir, Profesa Jay (Joseph Haule), Fid Q na wengineo wengi.

BREAKING : MFANYAKAZI AKUTWA AMEGANDA KWENYE FREEZER MWAKA 1 TANGU APOTEE

Image
Jeshi la Polisi nchini Lebanon limemkamata mwanaume mmoja anayejulikana kwa jina la Nader Essam Assaf ambaye amekutwa na mwili wa mfanyakazi wake wa ndani akiwa amekufa ambaye alikuwa ni raia wa Ufilipino. Mwili wa marehemu huyo Joanna Demafelis, 29, umekutwa ukiwa umewekwa kwenye jokofu (freezer) ndani ya nyumba ya mwajiri wake huyo, mwaka mmoja baada ya kuripotiwa kuwa amepotea katika mazingira ya kutatanisha. Kifo cha binti huyo kimesababisha vurugu nchini Ufilipino ambapo kumesababisha kufungwa kwa safari ya kwenda kufanya kazi Kuwait, Lebanon. Mtuhumiwa huyo Assaf na mkewe Mona wanatuhumiwa kuhusika na kifo hicho cha binti huyo. Hatahivyo mwanamke huyo bado hajapatikana kutokana na kwamba yuko mafichoni kufuatia tukio hilo.