Posts

Showing posts from June 5, 2017

TAARIFA MPYA ZA MTOTO DOREE WA AJALI YA LUCKY VICENT

Image
Mtoto Doreen Mshana, manusura wa ajali ya Lucky Vincent, ameruhusiwa kutoka Hospitali na sasa ameungana na wenzake wawili katika nyumba maalum wanamoishi, Marekani, jimbo la Iowa. Awali, wanafunzi wengine waliokuwa wakitibiwa katika Hospitali ya Mercy Hospital, Sioux City, Saidia Awadh na Wilson Tarimo, waliruhusiwa kutoka hospitali walimokuwa wakitibiwa. Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, ameandika katika ukurasa wake wa facebook na kueleza kuwa sasa Doreen, ameungana na wenzake baada ya hali yake kuimarika. Doreen, alibaki hospitali hapo kutokana na majereha makubwa aliyopata na hivyo kulazimika kufanyiwa upasuaji mkubwa wa uti wa mgongo. Wanafunzi hao walinusurika katika ajali ya basi la shule ya msingi ya Lucky Vincent, iliyoua wanafunzi 32, walimu wawili na dereva, Mei 6 mwaka huu, Karatu, Arusha.

Breaking News: Halim Mdee na Ester Bulaya wapewa adhabu ya kutohudhuria Bungeni mpaka mwakani

Image
Halima Mdee na Esther Bulaya wamehukumiwa kutohudhuria vikao vyote vya bunge linaloendelea mpaka mkutano ujao wa Bunge la Bajeti ya 2018/19. Hukumu hiyo imeungwa mkono na wabunge wengi waliopitisha azimio hilo. Mapema leo, Jumatatu Kamati ya Maadili  ilisema Bulaya na Mdee wamemaliza adhabu za kawaida zilizopo kwenye kanuni za bunge. Hata hivyo, Bunge liliendelea  kujadili makosa ya wabunge hao wa Bunda na Kawe. Mwenyekiti wa kamati hiyo, George Mkuchika aliliomba Bunge kujadili adhabu inayostahili kulingana na makosa yao. Kanuni inasema, mbunge anayefanya kosa la kwanza anaweza akazuiwa kuhudhuria vikao visivyozidi 10 na atayakosea kwa mara ya pili anaweza kuzuiwa kuhudhuria vikao visivyozidi 20.

Faida ya kula karoti

Image
Ulaji wa karoti kwa wingi, hasa karoti yenye hali ya ubichi husaidia kutibu magonjwa yafutayo; 1. Huongeza kinga za mwili. Pia ni chanzo kizuri cha vitamin na husaidia kuongeza kinga ya mwili hivyo kusaidia mwili kutopata magonjwa. 2. Husaidia kuona vizuri. vitamin A ambayo ina patikana kwa wingi husaidia kuongeza uwezo wa kuona na mawasiliano ya seli. Pia ina madini kama sodiam,sulphur,chlorine na iodine. 3. Husaidia matatizo kutibu matatizo ya ngozi. Juisi ya caroti husaidia sana katika kutibu ngozi iliyo kauka. 4. Kutibu vidonda vya tumbo. Ulaji wa mara kwa mara hupunguza uwezo wa kupata vidonda vya tumbo pamoja na madhara mengine kwenye mfumo wa chakula.

MSANII HARMONIZE WA WCBAACHIA PICHA HIZI NA MPENZI WAKE MPYA (+PICHAZ)

Image
Baada ya Kuachana na mrembo wa filamu Tanzania  Jacqueline Wolper , ilisemekana kuwa WCB super staa  Harmonize  anampenzi mpya, mzungu , ana pesa, kamnunulia gari Harmonize na anamjengea jumba kubwa huko Madale