Posts

Showing posts from December 1, 2017

FIFA YATANGAZA MAKUNDI YA KOMBE LA DUNIA MWAKA 2018

Image
FIFA limetangaza makundi ya michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika mwakani nchini Urusi. Makundi ya Kombe la Dunia 2018 Katika makundi hayo makundi yanayoonekana hatari zaidi ni Kundi C ambako kuna Ufaransa, Australia, Peru na Denmark na Kundi F linaloundwa na Ujerumani, Mexico, Sweden na Jamhuri ya watu Korea. Mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo utafanyika kati ya Mwenyeji, Urusi dhidi ya Saudi Arabia tarehe 24 juni 2018 kunako dimba la Luzhniki.

WEMA SEPETU ATANGAZA RASMI KURUDI CCM

Image
  Wema Sepetu wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. MSANII maarufu wa Bongo Movie, Wema Sepetu leo Ijumaa, Desemba 1, 2017 ametangaza rasmi kukihama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kurudi katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kile alichodai kuwa ni kukosa amani ndani ya chama hicho. Wema ambaye ni alikuwa mshindi namba moja wa Taji la Miss Tanzania 2006, amesema Chadema ni kama nyumba inayomkosesha amani hivyo hana haja ya kuendelea kuishi ndani ya nyumba hiyo.Amesisitiza kwake amani ni jambo kubwa sana hivyo anandoka ndani ya Chadema na kurejea nyumbani alikokulia kwa maana ya CCM. Wema na mama yake mzazi, Mariam Sepetu walihamia Chadema mwezi Februari mwaka huu baada ya kuhusishwa kwenye sakata la biashara ya madawa ya kulevya ambapo mpaka sasa kesi yake bado inaendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.