Posts

Showing posts from August 1, 2013

HIVI NDIVYO MPIGA PICHA WA NEW HABARI ALIVYO FANYWA WAKATI WA MAPOKEZI YA WAZIRI MKUU WA THAILAND UWANJA WA NDEGE DAR

Image
  Mpigapicha wa New Habari Anthony Siyame akidhalilishwa na askari wa Idara ya Usalama wa Taifa wakati wa mapokezi ya Waziri Mkuu wa ...Thailand Yungluck Shinawatra baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa JNIA. Cha ajabu ni kwanba wakati vyombo vya habari vijinyanyapaliwa na kukosa kufanya kazi yake kwa uhuru na uzarendo ndani ya nche yake zawa wanahabari wengine wakigeni walipewa ushirikiano kana kwamba ni miungu na kufanya kazi zao bila bughuza kwa kupiga picha hadi uvunguni kwa waziri mkuu huyo kutoka kwa wakulima mpunga Thailand. TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

AGNESS MASOGANGE AMPONZA MADEE NA KUSABABSHA AVULIWE NGUO AIRPORT

Image
Kwenye Exclusive interview na millardayo , Madee amehadithia kila kitu kilichomtokea wakati anaingia tu Afrika Kusini siku kadhaa zilizopita ambapo hii imetokea kutokana na ukubwa wa habari, uzito wa tukio la wale Watanzania wawili wasichana (Akina Masogange )  waliokamatwa kwenye kiwanja cha ndege Johannesburg wakiwa na dawa za kulevya wakitokea Tanzania. Madee anakwambia alipotua kwenye kiwanja cha ndege, kawaida huwa kuna utaratibu wa kuchekiwa hati ya kusafiria na ukaguzi mwingine ambao hufanywa na mitambo maalum kwa kila abiria anaeingia Afrika kusini, ni ukaguzi ambao unafanywa Airport kabla ya abiria kuruhusiwa kuingia kwenye nchi yenyewe. Kilichomfanya Madee kusachiwa na kuhojiwa karibu dakika 60 ni pale tu aliposema anatokea Tanzania, kuna wazungu wawili wenye sare tofauti za kipolisi wakaanza kumsachi mpaka kufikia kumwambia avue t shirt yake, alivua t shirt na kubakiwa na nguo nyepesi ya ndani wakati huo abiria wenzake aliokwenda nao walikua w...

"SIJUTII KUTIMULIWA BIG BROTHER, NAAMINI HAIKUWA RIZIKI YANGU"...NANDO

Image
Aliyekuwa mwakilishi wa Tanzania kwenye shindano la Big Brother Africa, Ammy Nando amesema hana majuto yoyote  baada ya kuondolewa kwenye shindano hilo. Nando ambaye aliondolewa wiki iliyopita kwa kuvunja  sheria za shindano hilo ,  leo amefunguka  kwa  mara  ya  kwanza ndani  ya  kipindi cha XXL cha Clouds FM. “I live my life with no regrets,” alisema Nando  na  kuongeza: “Sitaki kufikiria  matatizo wala nini, kilichotokea ndio kimetokea... "Najipanga upya ili  niendelee na maisha mengine. Vingapi vizuri  vimetokea nyuma ?  "Tokea  nilipokuwa mtoto mdogo nani alikuwa ananijua? Sasa hivi nipo peace , nashukuru kwamba mmenipokea vizuri.  "Naendelea na maisha, uzuri nimepata platform ya kutengezeza jina langu, kwahiyo naenda hivyo hivyo mpaka huko ntakapofika.”

MADENI YAMUUMBUA MSANII WA BONGO MOVIE....

Image
STAA wa filamu za Kibongo, Coletha Raymond ‘Koleta’ kwa mara nyingine tena amekumbwa na tuhuma za kukwepa kulipa deni la shilingi 400,000 analodaiwa na staa mwenzake, Husna Iddi ‘Sajenti’.. Kwa mujibu wa chanzo chetu, Koleta alikopa nguo kwenye duka la Sajenti kwa maelezo kwamba angelipa jioni ya siku hiyo lakini mpaka sasa ni miezi saba imepita bila msanii huyo kulipa deni hilo. Ikazidi kudaiwa kuwa hata Sajenti anapompigia simu Koleta ili kumuulizia kuhusu deni hilo, msanii huyo hapokei simu, hali inayotoa tafsiri kwamba anataka kumdhulumu. Mwandishi  wetu alimtafuta Sajenti ili kupata uhakika kama kweli anamdai Koleta ambapo alifunguka kama ifuatavyo:   “Sijawahi kumuona mtu msumbufu kama Koleta na sasa naanza kuamini maneno ya watu kwamba ana asili ya utapeli,” alisema Sajenti. Akaongeza kuwa anamdai  Koleta tangu mwaka jana na imefikia hatua sasa hapokei simu yake.    “Kinachoniuma ni pale anaposhindwa kupokea simu yangu, nikitumi...

MASAA 48 WALIYOPEWA WAASI WA M23 YAKO UKINGONI.....KICHAPO KITAANZA MUDA WOWOTE

Image
Muda wa saa 48 wa kusalimisha silaha kwa waasi wa March 23(M23), Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umemalizika na wakati wowote mapigano yanaweza kuanza. Misheni ya Kutuliza Amani ya Umoja wa Mataifa(Monusco) , ilitoa saa hizo zinazomalizika leo na Jeshi la UN litaanza kutumia nguvu kunyang’anya silaha waasi hao. Taarifa ya  Monusco iliyotolewa na Msimamizi wa Misheni hiyo, Luteni Jenerali Carlos Alberto dos Santos Cruz na kusambazwa na Idara ya Mawasiliano ya Umoja wa Mataifa jana, inaeleza kwamba, watu binafsi katika eneo la Kivu ya Magharibi ambalo linajumisha Goma na Sake na ambao hawahusiki na vyombo vya usalama wamepewa saa 48 kuanzia saa kumi jana (juzi) kwa saa za Goma (Jumanne) kuzisalimisha silaha zao. Taarifa ilisema, “Baada ya saa 10 jioni ya Alhamisi, Agosti Mosi, wale wote ambao watakuwa hawajasalimisha silaha zao watach...

KWELI HUJAFA HUJAUMBIKA...........: KANSA YA NGOZI YAMHARIBU MTOTO WA MIAKA 7....BABA AMWAGA MACHOZI AKIOMBA MSAADA

Image
MTOTO Ashura Mustapha (7) mkazi wa Mwandege, wilayani  Mkuranga, Pwani anasumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya ngozi tangu akiwa na mwaka mmoja. Akizungumza na mwandishi wetu, baba mzazi wa mtoto huyo, Mustapha Makombe alisema: “Mwanangu anateseka sana jamani, ugonjwa ulianza kama malengelenge akiwa na umri wa mwaka mmoja tukawa tunakwenda hospitali ndogondogo lakini baadaye tukaamua kumpeleka Muhimbili ambapo tulipewa barua ya kutuelekeza kwenda CCBRT, kule ndipo wakagundua mwanangu ana kansa ya ngozi steji ya nne. “Baada ya kuhangaika katika hospitali nyingi bila mafanikio, nikaamua kwenda Hospitali ya Regency (Dar) kuomba msaada wa kwenda kutibiwa India. “Pale waliniambia nichangie shilingi milioni moja na laki tano kwa ajili ya tiketi na viza ili mwanangu akatibiwe India, hizo hela mimi sina. Naomba Watanzania mnisaidie hata kwa fedha za mitandao kwa namba 0769 517765 na 0715 424697 ili niweze kumpeleka mwanangu India akatibiwe,” alisema baba mzazi.

CHUMBA ALICHOPELEKWA ROSE NDAUKA CHAKUTWA NA KONDOMU TANO ZILIZOTUMIKA

Image
  Chumba cha hoteli ambacho Rose Ndauka  alinaswa  akiingia  na  dogo  Nasry  ambaye  ni  msanii  wa  bongo  fleva, kimekutwa  na  kondomu  tano  zilizotumia... Rose  Ndauka  ambaye  ni  mchumba  wa  Malik  Bandawe,wiki  iliyopita  alinaswa  akiingizwa  katika  chuba  hicho na  msanii Nassoro Ayoub  "Nasry".     Kwa  msaada  wa  wafanya  usafi  wa  hoteli  hiyo  iliyoko  maeneo  ya  kinondoni  jijini  Dar,wawili  hao  waliingia  katika  chumba  namba G17   cha  hoteli  hiyo  na  kutumia  masaa  takribani  matatu  huku  chumba  kikiwa  kimefungwa  na  walipotoka  chumba kilikuwa  hoi  bin  taaban.... "Mimi  ndiye  ...

CHAMA CHA RAIS MUGABE CHAJITANGAZIA USHINDI ...

Image
Chama cha Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, ZANU -PF leo kimesema kimeibuka na ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi uliofanyika jana. Ushindi huo utamfanya Mugabe aiongeze nchi hiyo kwa miaka mitano mingine. Hata hivyo mpinzani wake wa karibu amesema kura zimeibiwa.Matokeo rasmi ya uchaguzi huo yanatarajia kutangazwa August 5. Chanzo kilicho karibu na Mugabe mwenye umri wa miaka 89, kimeiambia Reuters kuwa majibu yako wazi.   “Tumeshinda uchaguzi. Tumeizika MDC. Hatukuwa na mashaka yoyote kuhusu kushinda,” kilisema chanzo hicho.   Akijibu madai hayo, waziri mkuu nchi hiyo Morgan Tsvangirai ambaye ni mpinzani mkuu wa Mugabe kwenye uchaguzi huo, ameuelezea kama wa ulaghai. MDC kilipanga kuwa na mkutano wa dharura leo.