ANGALIA PICHA ZA UTENGENEZAJI WA FILAMU MPYA YA WASTARA BAADA YA MATATIZO
Hatimaye mwadadada Wastara Sajuki amerejea tena kwenye ulimwengu wa filamu baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu kwenye tasnia hii kutokana na matatizo aliyoyapata ya kuondokewa na mumewe Juma Kilowoko (Sajuki) mnamo mwezi waJanuary mwaka huu. Akizungumza katika utengenezaji wa Filamu yake mpya ya kwanza atakayoiachia wastara amesema Filamu hii mpya wastara amesema kuwa itahusu maisha ya kawaida ya mwanadamu na jinsi ambavyo matatizo yanayomkabili binadamu yanavyoweza na kumuathiri kisaikolojia na kumpelekea kufanya mambo ambayo hakuwai kuyafikiria. Wastara amesema kisa kikuu kwenye filamu hii yake mpya ni jinsi familia moja iliyokuwa na maisha mazuri na baadaye mama wa familia kupata kansa ya kizazi na kupelekea kuondelewa kizazi chake kabla ya kufiwa na mtoto wake pekee aliyekuwa naye na namna ambayo mumewe anavyojaribu kumliwaza mkewe kwa matatizo yanayotokea. Wastara amesema kuwa kwenye Filamu hii...