Posts

Showing posts from September 7, 2017

Kanisa la Askofu Gwajima labomolewa

Image
Dar es Salaam. Kanisa la Ufufuo na Uzima lililopo Mbezi Inn linalomilikiwa na Askofu Josephat Gwajima limebomolewa. Nyumba hiyo ya ibada ambayo pia ilikuwa ikitumika kama kituo cha maombezi imebomolewa na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads). Imeelezwa kanisa hilo limejengwa ndani ya hifadhi ya Barabara ya Morogoro ya mita 121.5. Kwa mujibu wa waumini wa kanisa hilo, pia limekuwa likitumika  kama kituo cha kufundishia wachungaji limebomolewa jana jioni hali iliyosababisha waumini wa Kanisa hilo kusalia nje. Mwananchi imefika katika kanisa hilo na kukuta  vitu vikiwa nje na baadhi ya waumini wakiendelea  na maombi nje. Mmoja wa waumini ambaye hakutaka kujitambulisha kwa madai si msemaji, amesema kanisa leo limebomolewa lakini injili inaendelea kuhubiriwa kama kawaida . "Tunaendelea na huduma na kesho tutakuwa na ibada itakayoanza saa kumi jioni "amesema. Muumini mwingine pia amesema hali ilikuwa mbaya jana wakati kanisa hilo linabomolewa kwani ...

Kauli ya Rais Magufuli Baada ya Kupata Taarifa za Lissu

Image
RAIS John Magufuli ameeleza kusikitishwa kwake kutokana na kushambuliwa kwa kupigwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema). “Nimepokea kwa masikitiko tukio la kupigwa risasi Mh.Tundu Lissu, namuombea kwa Mwenyezi Mungu aweze kupona haraka. Aidha, vyombo vya dola viwasake wale wote waliohusika na tukio hili la kinyama na kuwafikisha ktk mikono ya sheria,” amesema Rais Magufuli. Stori zinazo husiana na ulizosoma

BREAKING: Tundu Lissu Apigwa Risasi

Image
MBUNGE wa Singida Mashariki, Mwanasheria Mkuu wa Chadema na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Tundu Lissu amevamiwa na watu wasiojulikana kisha kumpiga risasi zinazodaiwa kuwa tano. Tukio hilo linadaiwa kutokea leo akiwa nyumbani kwake Area D Mjini Dodoma ambapo watu hao walimvamia akiwa kwenye gari kisha kumpiga risasi za miguuni na tumboni. Imeelezwa kuwa alikuwa akitokea Bungeni na alienda Nyumbani kula chakula cha mchana.  Dereva wake akiwa ameshika nguo na viatu vya Tundu Lissu Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema kuwa Mh. Lissu amepigwa risasi zaidi ya mbili alipokuwa amweetoka bungeni na kwenda nyumbani kwakwe kwa ajili ya chakula cha mchana. Gari la Mbunge Lissu likionekana na baadhi ya matundu zilipopigwa Risasi  Kwa mujibu wa taarifa zilizopo ni kwamba amekimbizwa hospitali na sasa yupo chumba cha upasuaji. "Hli ya Tundu Lisu ni mbaya ...

Kutajwa Sakata la Madini… Waziri Simbachawene, Ngonyani Wajiuzulu

Image
Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene. WAZIRI wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) , George Simbachawene na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani wameandika barua za kujiuzulu nyadhifa hizo ili kupisha uchunguzi baada ya kutajwa kuhusika kwa ubadhilifu kwenye Ripoti za Uchunguzi wa Biashara ya Madini ya Almasi na Tanzanite. Uamuzi a viongozi hao umekuja ikiwa ni dakika chache baada ya Rais Magufuli kupokea Ripoti hiyo kutoka kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambapo Rais aliwataka viongozi wote wa serikali walioko madarakani na wametajwa kuhusika kwenye kashfa hizo waachie ngazi ili kupisha uchunguzi wa vyombo vya usalama. Kwa upande wake, akiongea na Mwananchi leo Alhamisi mchana mara baada ya hafla ya makabidhianao ya ripoti hizo, Ngonyani amesema amepokea kauli ya Rais kwa mikono miwili na sasa anaandika barua ya kujiuzulu nafasi hiyo. Naibu Waziri w...

Breaking News: Mtekaji Wa Watoto Arusha Auawa Kwa Kupigwa Risasi

Image
Mtuhumiwa Samson Petro enzi za uhai wake. Kijana aliyehusika na matukio ya utekaji watoto mkoani Arusha, Samson Petro (18) amefariki dunia kwa kupigwa risasi na polisi. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amethibitisha kutokea kwa kifo hicho alipozungumza na waandishi wa habari. Kamanda Mkumbo amesema kijana huyo ambaye alikamatwa mkoani Geita alikokuwa amekimbia kabla ya kurejeshwa Arusha alitaka kukimbia alipokuwa anakwenda kuwaonyesha polisi watuhumiwa wenzake wa utekaji  saa tano usiku wa jana Jumatano. Hivi karibuni alipokamatwa mkoani Geita, kijana huyo ambaye sasa ni marehemu alikiri kuwateka watoto wanne mkoani Arusha baada ya kukamatwa mjini Katoro wilayani Geita alikotekeleza tukio lingine la utekaji. Akizungumza akiwa chini ya ulinzi wa polisi wiki iliyopita, kijana huyo alisema watoto wawili aliwarudisha kwa wazazi wao baada ya kupewa Sh300,000. Alisema wengine wawili aliwatelekeza mtaani baada ya wazazi wao kutotoa kiasi cha fed...