VIONGOZI MBALI MBALI WASHIRIKI KUAGA MWILI WA MHE. EUGEN MWAIPOSA ALIYEKUWA MBUNGE WA UKONGA - DAR
Mwili wa marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga ukiwasili kwenye viwanja vya bunge leo mjini Dodoma kwa ajili ya kuagwa. Wabunge Mhe. Anna Abdalla (kushoto) na Mhe. Ester Bulaya wakiaga mwili wa marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa aliyekuwa mbunge wa Ukonga kwenye viwanja vya bunge jana mjini Dodoma. Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge Wanawake Mhe. Anna Abdallah akimfariji mume wa marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa mbunge wa Ukonga aliyefariki usiku wa kuamkia Juni 2 nyumbani kwake mjini Dodoma. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Ombeni Sefue, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai, Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda, Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu, Mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bibi Chiku Galawa wakiwa kwenye shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Mhe. Eugen Mwaiposa. Baadhi ya Wabunge wakiwa kwenye hali ya majonzi mara baada ya kuwasili kwa mwi...