Lusekelo: Tusimtumie Lissu kupata umaarufu
Mchungaji Lusekelo ameandika ujumbe huo kupitia kwenye mitandao yake ya kijamii na kusema kuwa mbona watu hao hawakuonekana kulaani mauaji ya Kibiti au kuitisha maombezi baada ya watu Kibiti kuuawa. "Tusitumie tatizo la ndugu yetu Tundu lissu kujipatia umaarufu wa kisiasa au wakidini, mtu yeyote ambaye anatumia tukio hili kujipatia umaarufu wa kisiasa au wakidini namfananisha na wale wahuni ambao basi likianguka anaenda kuchukua simu kwanza, ni jambo ovu sana wewe unakuwa ni sehemu ya watu walio mpiga risasi Tundu lissu. Mwenzako anaumwa wewe unatumia ugonjwa wake kujipatia umaarufu wa kidini au wakisiasa ni jambo baya sana, mbona sikusikia wakilaani mauaji ya kibiti au kuitisha maombezi watu wakibiti walipo uwawa, mbona hawaja laani utekaji na mauaji ya watoto Arusha hata wa Marekani (umoja wa ulaya) sikusikia wanalaani mauaji ya kibiti" aliandika Mzee wa Upako Aidha Mchungaji huyo amesema kuwa yeye anaamini watu hao wanatumia matatizo ya Tundu Lissu...