RAIS KIKWETE AWAPA POLE MAJERUHI YA MSONGAMANO WA WANANCHI BAADA YA MKUTANO WA KAMPENI KATIKA UWANJA WA JAMHURI MJINI MOROGORO JANA
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro Dkt. Ritha Lyamuya alipokwenda kuwapa pole majeruhi walioumia katika msongamano mkubwa uliotokea katika mlango wa kutokea nje baada ya mkutano wa kampeni wa CCM katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana Septemba 6, 2015. Watu wawili walipoteza maisha, akiwemo mvulana wa miaka 12 aliyejulikana kwa jina la Ramadhani Abdallah na mwanamama Grace George (42), ambapo jumla ya watu 17 walijeruhiwa na kukimbizwa hospitalini hapo. Hadi jioni hii majeruhi saba walikuwa wameruhusiwa. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Kaimu Mganga Mku wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro Dkt. Samson Tarimo alipokwenda kuwapa pole majeruhi walioumia katika mlango wa kutokea nje baada ya mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana Septemba 6, 2015. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mweka Hazina wa CCM mkoa wa Morogoro Ndg. Ha...