BREAKING NEWS: MUGABE ANG’OLEWA UENYEKITI WA ZANU-PF
Chama tawala nchini Zimbabwe, ZANU-PF, kimemtimua Rais Robert Mugabe, kwenye uenyekiti wa chama na kumteua aliyekuwa Makamu wa Rais kabla ya kufutwa kazi na Mugabe, Emerson Mnangagwa kuongoza chama hicho.Anatakiwa ajiuzulu mwenyewe urais au kung’olewa madarakani kwa lazima kwa kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye na Bunge la nchi hiyo. Vilevile chama tawala ZANU-PF kimemfutia uanachama mke wa Rais Mugabe, Grace Mugabe. Hatua hiyo inamnyang’anya moja kwa moja cheo cha uenyekiti wa Baraza la Wanawake la chama hicho. Kikao cha Kamati Kuu ya chama tawala nchini Zimbabwe, ZANU-PF kinaendelea muda huu huku lengo ni kumng’oa madarakani Rais Robert Mugabe aliyedumu kwa miaka 37. Washiriki wa karibu wa Rais Robert Mugabe katika chama alichokianzisha wamemtaka kiongozi huyo kuondoka madarakani kufuatia shinikizo kubwa la maandamano linaloendelea nchini humo sanjari na jeshi kuingilia kati. Katika kikao hicho kinachoendelea leo, Novemba 19, viongozi wa juu wa chama hich...