Emmanuel Mbasha asema bado anamuhitaji mke wake Flora ingawa anadai amezaa nje ya ndoa
Msanii wa muziki wa Injili, Emmanuel Mbasha amesema bado anamuhitaji aliyekuwa mke wake Flora Mbasha ingawa anadai tayari ameshazaa nje ya ndoa na mwanaume mwingine. Muimbaji huyo amedai ameshafanya jitihada mbalimbali bila mafanikio kwa kipindi cha miaka miwili ili kurudiana na mama watoto wake huyo. “Moyo wa kurudiana nilikuwa nao sana, tena sana, ikiumbukwe mambo yametokea 2014, mwaka huo mzima nilikuwa namuomba Flora rudi nyumbani tuendelee na maisha, 2015 nikaendelea kumuomba rudi nyumbani tuendelee na maisha. Tumeitisha vikao vya kila aina ili kusuluishwa lakini bado amekuwa mgumu lakini nadhani tayari alishapanga haya yatokee ndio maana akaamua yeye kuniacha mimi nilikuwa sina mpango huo,” Emmanuel Mbasha alikimbia kipindi cha Enewz cha EATV.. “Mimi sijaachana naye, sema tumetengana na kipindi tumetengana amepata mtoto labda kuna kitu anaogopa, lakini mimi sina tatizo naye, Flora mimi nakuhitaji rudi nyumbani tuendelee na maisha,” aliongeza. Muimbaji h...