Posts

Showing posts from August 13, 2016

Yanga yashinda bao 1-0 dhidi ya Mo Bejeia

Image
Straika mpyawa Yanga, Obrey Chirwa (katikati) akiwatoka wachezaji wa Mo Bejaia. Kikosi cha Mo Bejaia wakipasha kabla ya mechi. Kikosi cha Yanga wakipasha kabla ya mechi. TIMU ya Yanga imeshinda bao 1-0 dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria katika Kombe la Shirikisho Afrika, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam  na kufikisha point 4.  Bao la Yanga limefungwa kipindi cha kwanza Dakika ya pili na Amissi Tambwe. Kikosi cha Yanga SC; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul/Said Juma ‘Makapu’ dk46, Mwinyi Mngwali, Andrew Vincent ‘Dante’/Kevin Yondan dk17, Vincent Bossou, Mbuyu Twite, Simon Msuva, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe, Obrey Chirwa na Deus Kaseke/Juma Mahadhi. MO Bejaia; Chamseddine Rahmani, Ismail Benettayeb, Faouzi Rahal, Sofiane Khadir, Soumaila Sidibe, Zakaria Bencherifa, Mohamed Yacine Athmani, Morgan Betorangal, Sofiane Baouali, Amar Benmelouka na Kamel Yesli.

VERA SIDIKA AELEZA SABABU NA KIASI ALICHOTUMIA KUONGEZA MATITI YAKE

Image
Mrembo maarufu kutoka Kenya,Vera Sidika ameweka wazi kuwa alifanya plastic surgery ili aweze kuwa na matiti makubwa. Vera aliyasema hayo akiwa kwenye mahojiano ya Tv na kipindi cha FNL cha EATV ambapo alieleza kuwa alifikia uamuzi huo baada ya kuona sehemu zingine za mwili wake ni kubwa kasoro matiti,hivyo akaamua kutafuta mwili wenye uwiano. “Kipindi nakua kutoka utotoni na kuwa kijana,mwili wangu ulianza kuwa mkubwa na ukaanza kuwa mkubwa sehemu nyingine huku kwa juu nikawa kama nimenyimwa kidogo,halafu kwenye industry kama hollywood sio big deal,watu wanafanya surgery kama kawaida ila kwa Afrika ni kitu kipya..Nilifanyiwa surgery ya matiti,inaitwa boob job,nilikuwa nataka niwe na mwili wenye uwiano,nilifanyiwa Marekani mjini hollywood na iligharimu kama dola elfu 30” alifunguka vera sidika ambaye pia alidai kuwa uamuzi huo ulichangiwa na ukweli kwamba alitaka avutie zaidi kwenye show biz na kuongeza kuwa hela alizotumia kufanya plastic surgery zinarudi kutokan

Fidel Castro Agonga Miaka 90

Image
Fidel Castro RAIS wa zamami wa Cuba na Kiongozi mwanamapinduzi, Fidel Castro anasherehekea kutimiza miaka 90 tangu kuzaliwa kwake. Fidel Castro alizaliwa Agosti 13, 1926  huko Birán nchini Cuba na aliyetawala Kisiwa hicho kwa zaidi ya miaka 50, hajaonekana hadharani kwa miezi mingi na bado haijabainika iwapo atajitokeza leo. April 19, 2011, Fidel Castro, kushoto, akinyanyua mkono wa mdogo wake, Rais wa Cuba, Raul Castro, wakati wa Mkutano wa Chama cha Congress, Havana, Cuba. Ingawa Cuba imebadilika sana tangu mdogo wake, Raul Castro achukue madaraka miaka nane iliyopita, na ushawishi wa Fidel umeshuka, bado anaenziwa sana na raia wengi wa Cuba. Raul alizaliwa mnamo June 3, 1931 huko huko Birán nchini Cuba Picha za Fidel Castro, kuanzia kushoto akiwa Havana Aprili 29, 1961 kuzungumza na wanahabari, Washington, D.C., Aprili 6, 2000 na Februari. 13, 2016. Hakuna hafla yoyote rasmi iliyopangiwa kufanywa, lakini Rais wa Venezuela Nicolas Maduro, taifa mshirika