HOTUBA YA BAJETI YA SERIKALI KWA MWAKA 2014/2015
Waziri wa Fedha, Saada Mkuya (MB) akiwasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yake kwa mwaka 2014/15 . UTANGULIZI 1.Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu lijadili na kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka 2014/2015. Pamoja na hotuba hii, nimewasilisha vitabu vinne vinavyoelezea kwa kina takwimu za Bajeti. Kitabu cha Kwanza ni makisio ya mapato; Kitabu chaPili ni makisio ya matumizi ya kawaida kwa wizara, idara za Serikali zinazojitegemea, wakala na taasisi za Serikali; Kitabu cha Tatu ni makisio ya matumizi ya kawaida kwa mikoa na mamlaka za serikali za mitaa; na Kitabu cha Nne ni makadirio ya matumizi ya maendeleo kwa wizara, idara za Serikali zinazojitegemea, wakala na taasisi za Serikali, mikoa na mamlaka za serikali za mitaa. Aidha, upo Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2014 ambao ni sehemu ya bajeti hii. <<BOFYA HAPA...