Fahamu mbinu 10 za vigogo kusafirisha unga
Viatu vya kimasai na zana nyingine zinazotumika kama urembo ambavyo vimetajwa kama zana muhimu zinazotumiwa katika usafirishwaji wa madawa hayo. Stori: Makongoro Oging’ na Issa Mnally, UWAZI DAR ES SALAAM: Jeshi la Polisi Tanzania kwenye viwanja vya ndege vilivyopo nchini limekuwa likipambana na wauza madawa ya kulevya ‘unga’ kwa kugundua na kuzima mbinu zote wanazotumia kusafirisha biashara hiyo haramu, hivyo kupunguza kasi ya uingizwaji na utoaji wa unga kwa njia ya ndege, UWAZI limeambiwa. Akizungumza na gazeti hii katika mahojiano maalum yaliyofanyika wiki iliyopita Makao Makuu ya Polisi wa Viwanja vya Ndege Tanzania yaliyopo jijini Dar, Kamanda wa Viwanja vya Ndege, ACP Martin Otieno (pichani) alizitaja mbinu kumi wanazotumia wauza unga hao kusafirishia bidhaa hiyo. “Kwanza napenda kuweka wazi kuwa, kwa sasa hatuna mchezo na wauza unga. Mbinu zao zote wanazotumia kusafirishia madawa yao tunazijua. Na napenda kuchukua nafasi hii kuwaambi...