HISTORIA MPYA YAANDIKWA HATIMAYE NGWEA AZIKWA NA MAELFU YA WATU KWENYE MAKABURI YA KIHONDA MKOANI MOROGORO....
PICHA ZA MAZIKO YAKE HII NDO NYUMBA YA MILELE YA NGWEAR. Baada ya siku kadhaa zilizokuwa na kila aina ya harakati, ugumu na majonzi makubwa, Albert Mangweha aka Ngwair leo amezikwa kwenye makaburi ya Kihonda mkoani Morogoro ambako ni nyumbani kwao. Kabla ya kuzikwa, wananchi wa Morogoro walipata fursa ya kuuaga mwili wake kwenye uwanja wa Jamhuri. Umati mkubwa wa wananchi ulijitokeza kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa Ngwair aliyefariki nchini Afrika Kusini, wiki iliyopita. Wasanii wengi kutoka Dar es Salaam nao wamehudhuria mazishi hayo.“Marehemu Albert Mangweha azikwa kishujaa sana ni um...