Posts

Showing posts from March 9, 2017

SAIDA KAROLI ASIMULIA JINSI ALIVYOIBIWA KAZI ZAKE KISA KUTOJUA KUSOMA NA KUANDIKA

Image
Jana kupitia kipindi cha Take One cha Clouds TV, mtangazaji Zamaradi alimuhoji mwimbaji wa muziki wa asili Saida Karoli ambapo alikiri kuwa hana haki kwenye nyimbo zake kutokana na mikataba aliyosainishwa na Meneja wake sababu na yeye hakuwa anajua kusoma na kuandika na akadai zaidi ya album tano hana haki nazo na meneja wake wa zamani ndio mwenye haki nazo .Kingine alichozungumza Saida ni kuhusu wimbo wa Salome ambao Diamond Platnumz aliurudia ambapo alisema ana hesabu kama alitoa bure kwani hata fedha aliyopewa ni kidogo na haifai kuongelea. ”Siwezi kulalamika hata kidogo, mara nyingi naulizwa nasema sina tatizo, sina haki na zile nyimbo maana yeye ndio alinipa mikataba na yeye ndio alinitengenezea, hata hii ya Diamond naweza nikasema ikawa mbaya zaidi maana fedha niliyoipata siyo ya kuongelea, kwahiyo mimi najiona nimetoa bure”Waandishi kila siku wanakuwa wananiuliza nawambia nimempa Diamond nyimbo bure na nimetoa kwa moyo mmoja kweli, roho yangu moja ...

Paul Makonda Aenda Mapumziko ya Miezi Miwili South Africa

Image
Wakati utata ikigubika kuhusu safari ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwenda nchini Afrika Kusini, imebainika kuwa kiongozi huyo atakuwa likizo nchini humo kwa zaidi ya miezi miwili. Kwa mujibu wa habari iliyoandikwa katika gazeti la TanzaniaDaima imeeleza uwepo wa RC Makonda nchini Afrika Kusini ndio sababu ya kushindwa kuhudhuria sherehe ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Dunia ambapo ilitangazwa kuwa angekuwa mgeni rasmi katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Mwembeyanga. Kuondoka kwake nchini kumekuwa kwa kutatanisha wakati mamlaka husika zikishindwa kutoa taarifa kamili kuhusuana na safari yake. Wadadisi wa mambo wanahoji uhalali wa Makonda kupewa mapumziko hayo nje ya nchi huku serikali ilitangaza kuzuia ziara zote za watumishi nje ya nchi ili kubana matumizi. Kutokana na zuio la safari za nj...

Tundu Lissu Afunguka Baada ya Kusikia Mwakyembe Amemzuia Kugombea Nafasi ya Rais wa TLS

Image
Anaandika Wakili Msomi Tundu Lissu: Waheshimiwa mawakili na wananchi wa nchi yetu. Nimesoma taarifa katika magazeti kadhaa ya leo kwamba Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison George Mwakyembe amenizuia kugombea nafasi ya Rais wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS). Kama taarifa hizo ni za kweli basi naomba kuweka masuala yafuatayo wazi: (1) Waziri wa Sheria na Katiba hana mamlaka yoyote, kwa mujibu wa Sheria iliyoanzisha TLS na kanuni zake, ya kuzuia ama kuruhusu mwanachama yeyote wa TLS kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya TLS. Hivyo, kama kweli Dkt. Mwakyembe ametoa kauli hiyo, basi huo utakuwa uthibitisho wa ama upungufu mkubwa wa uelewa wa Sheria au hulka ya ukiukaji wa sheria (culture of impunity) ambayo imeshamiri sana katika utawala huu wa sasa. (2) Mamlaka pekee inayohusika na uchaguzi wa TLS ni Kamati ya Uteuzi (Nominations Committee) ambayo ilikwishafanya uteuzi wa wagombea wote kwa kuzingatia sifa na vigezo vilivyowekwa na Sheria na Kanuni za...