Wivu wa Mapenzi Wasababisha Mauaji ya Kinyama ya Watu wawili
Watu wawili wamefariki dunia na mwingine mmoja kujijeruhi baada ya kutokea ugomvi unaohusishwa na wivu wa mapenzi mjni Bunda. Tukio hilo lilitokea jana saa tano asubuhi katika Mtaa wa Bunda Stoo baada ya mtu mmoja kuwavamia watu wawili kisha kuwachoma visu kabla ya kujichoma mwenyewe. Akizungumza mjini hapa, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Jaffari Mohamed alisema jana kuwa waliouawa ni Daudi Phares (29) mkazi wa Bunda na msichana aliyetambulika kwa jina moja la Monica (22) mkazi wa Magu mkoani Mwanza. Kamanda huyo alimtaja aliyejijeruhi baada ya kujichoma kisu maeneo mbalimbali mwilini mwake kuwa ni Selemani Jeremia (33) ambaye ni mkazi wa Magu. Alisema kuwa siku ya tukio Selemani alisafiri kutoka Magu mkoani Mwanza hadi Bunda ambapo alifika nyumbani kwa Daudi na kumkuta akiwa na Monica. Baada ya kufika nyumbani hapo Selemani alianza kumchoma visu Dauidi katika sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwamo kifuani upande wa kushoto na kusababisha ki...