Posts

Showing posts from February 25, 2016

BREAKING NEWZ: Mwanamuziki Mkongwe Kassim Kapili Afariki Dunia

Image
Mwanamuziki mkongwe wa muziki dansi Kassim Mapili akicharaza nyuzi za Gitaa lake chini ya Kundi zima la Mjomba Band . MWANAMUZIKI mkongwe wa muziki dansi Kassim Mapili amefariki dunia akiwa chumbani kwake, Tabata jijini Dar es Salaam. Katibu mkuu wa Chama cha Muziki wa Dansi (CHAMUDATA) Hassan Msumari, amesema kuwa kifo cha Mapili kimegunduliwa usiku huu baada ya mlango wa chumba chake kuvunjwa. Mlango huo ulivunjwa baada ya Kassim Mapili kutoonekana tangu alipokwenda kutazama mpira wa Arsenal na Barcelona Jumanne usiku. Kwa mujibu wa Msumari, mara mlango ulipovunjwa Kassim Mapili alionekana akiwa ameshafariki akiwa amejifunga taulo, ishara inayoonyesha kuwa aidha alikuwa anakwenda kukoga au ametoka kukoga. Jumatatu jioni Kassim Mapili alishiriki vizuri mazishi ya mwanahabari Fred Mosha makaburi ya Kinondoni ambapo alipewa wasaa wa kuongea machache na kama vile hiyo haitoshi, Mapili aliimba makaburini hapo kuomboleza kifo cha Fred Mosha.

Lulu adaiwa kulipiwa mahari

Image
= Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’. Dar es Salaam: Wakati akikanusha vikali taarifa mbaya za kuzushiwa kifo mwishoni mwa wiki iliyopita na watu ambao alisema hajui lengo lao, habari ya heri ni kwamba, staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, (pichani) anaelezwa kuwa kwenye shamrashamra za ndoa baada ya kudaiwa kulipiwa mahari na mfanyabiashara maarufu jijini Dar (jina linahifadhiwa kwa sasa). Kwa mujibu wa chanzo chetu makini ambacho ni mtu wa karibu wa Lulu, hivi karibuni mrembo huyo alilipiwa mahari hayo kwa siri kwa kuwa mwanaume huyo hakutaka mambo hayo yafike kwenye vyombo vya habari. “Sasa mimi nawapa habari motomoto kuwa Lulu amelipiwa mahari na mwanaume wake wa sasa lakini ishu nzima ilikuwa kwa siri sana,” kilidai chanzo hicho na kuongeza: “Shughuli nzima ilifanyika nyumbani kwa Lulu (Mbezi-Beach, Dar) na sasa kinachoendelea ni taratibu za harusi lakini jamaa (huyo mwanaume) hataki iwe na mbwembwe. Lulu akiwa katika poz...

Cement ya Dangote Yaanza Kusambaza Tanzania... Bei ya Mfuko Mmoja wa Cement yatajwa

Image
Kile kiwanda kikubwa cha Africa mashariki na Africa kwa ujumla kwa mara ya kwanza kimeanza kuzalisha kusambaza cement yake tar 21/02/ 2016. Kiwanda hicho ambacho ni tegemeo jipya kwa waakazi wa mikoa kusini Mtwara na Lindi kiliahidi ajira nyingi ya wakaanzi wa mikoa hiyo na watanzania kwa ujumla Cement tayari iko maduka kwa bei nafuu ya sh 13,500 tofauti na cement ya viwanda vingine. Tunawakaribisha wateja wa cement hiyo na wenye magari makubwa kufungua office mkoani Mtwara ili kuongeza ajira za madereva hapa mkoani TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Shuhudia Red Carpet ya Tuzo za Brit jana (Picha)

Image
Usiku wa kuamkia leo ulikuwa mzuri kwa mastaa kibao wa muziki wa Pop na Hip Hop duniani kutokana na tuzo za dunia za Brit zilizotangazwa katika Ukumbi wa London’s O2 Arena, Uingereza. Nimekuletea picha ‘red carpet’ katika tuzo hizo ambazo zilifunikwa kwa shoo ya nguvu kutoka kwa Adele, Rihanna na Drake.

Naibu Spika Dr Tulia Anusurika Kifo Baada ya Kupata Ajali Mbaya ya Gari....Nimekuwekea Picha za Ajali Hapa

Image
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson amenusurika kifo baada ya gari alilokuwa akisafiria kupata ajali jana jioni. Taarifa za awali zimeeleza kuwa Dk. Tulia alipata ajali hiyo baada ya gari dogo kugonga gari alilokuwa akisafiria katika eneo la Kiwira jijini Mbeya.

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI TAREHE 25.02.2016

Image

MAGAZETI YAUDAKU LEO trh 25/2/2016

Image

MAGAZETI YAMICHEZO NA BURUDANI

Image