Posts

Showing posts from October 3, 2018

Msigwa Kumburuza Mahakamani RC Hapi

Image
Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa amesema  atamfikisha mahakamani Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi  kufuatia uamuzi wake wa kumuweka ndani diwani wa Viti maalum CHADEMA, Silestina Jonso. Msigwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Iringa jana Octoba 2, alisema Hapi alimdhalilisha diwani huyo. “Alidiriki kumdhalilisha diwani wetu, sheria iko wazi sana, vipengele vyote vile mkuu wa mkoa hakufuata, amekiuka, ametoa amri ya kumpeleka diwani wetu polisi kinyume cha sheria. “Sasa kwa sababu amekiuka taratibu, mimi kama mwenyekiti wa kanda na mbunge ili kukomesha tabia hii ya RC Hapi  tumwambie hatukubaliani naye na hatujalala, anakuja na sheria zake za kutisha watu na kuwatia ndani. "Tumejipanga vizuri tunamfungulia kesi mahakamani kwa sababu anatumia madaraka yake vibaya. Tutakutana naye mahakamani kwa sababu anatumia madaraka vibaya.” Alisema Msigwa

Nafasi za Kazi zilizotangazwa Leo Aug 3

Image
Bonyeza links zifuatazo kusoma zaidi na kuapply 20 Field Marketing Representatives Jobs at MoGo Tanzania Limited 8 Jobs at Tanzania National Roads Agency (TANROADS) 4 Jobs at Zanzibar University Marketing Manager Job at Transsnet Financial Team Leader at KPMG’s International Development Advisory Services (IDAS) Shop Manager at Miniso Tanzania Company Limited Area Manager at at Miniso Tanzania Company Limited Training and Development Officer at Miniso Tanzania Company Limited Nafasi zingine ingia  www.ajirayako.co.tz

KUVISHWA PETE YA UCHUMBA, SIRI 3 KILIO CHA LULU ZAFICHUKA

Image
Elizabeth Michael ‘Lulu’ kuvishwa pete ya uchumba na Francis Shiza ‘Majizo B AADA ya wikiendi iliyopita staa ‘grade one’ wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kuvishwa pete ya uchumba na bosi wa Radio EFM, Francis Shiza ‘Majizo’ na kuangua kilio cha aina yake, siri tatu (3) zimefichuka, Risasi Mchanganyiko linakupa habari kamili. Kwa mujibu wa mtu aliyehudhuria, shughuli hiyo iliyofanyika nyumbani kwa Majizo, Mbezi-Beach jijini Dar ilikuwa ya aina yake kwani watu walifurahi kwa kula na kunywa huku mastaa wa filamu wakionekana kutoalikwa au kutokuwepo. “Unajua ishu ya Lulu kuvishwa pete ya uchumba ilikuwa ni siri sana ndiyo maana hakukuwa hata na mastaa wenzake wa filamu zaidi ya mwigizaji Mahsein Awadhi ‘Dk Cheni’ ambaye alikuwa mshehereshaji lakini ilifana kwani mpaka Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda alikuwepo,” alieleza mtu huyo kwa sharti la kutotajwa gazetini. SHEREHE ILIKUWA HIVI Chanzo kiliendelea kutiririka kwamba sherehe ilianza vizuri ...