CLINTON KUSHUHUDIA DONALD TRUMP AKIAPISHWA MAREKANI
Hillary Clinton na mumewe Bill wamethibitisha kwamba watahudhuria sherehe ya kuapishwa kwa rais mpya wa Marekani Donald Trump mjini Washington DC. George W Bush na mkewe Laura pia wametangaza kwamba wanapanga kuhudhuria sherehe hiyo mnamo tarehe 20 Januari. Wamesema wanataka "kushuhudia kukabidhiwa madaraka kwa rasi mwingine kwa njia ya amani." Tajiri huyo kutoka Manhattan, New York ataapishwa kuwa rais wa 45 wa Marekani katika makao makuu ya serikali Capitol Hill. Bw Trump alimshinda Bi Clinton katika uchaguzi mkuu uliofanyika Novemba mwaka jana na amemkosoa Bw Bush kutokana na vita vya Iraq na mashambulio ya 9/11. Kabla ya tangazo hilo la Jumanne, Jimmy Carter alikuwa ndiye rais wa zamani pekee aliyekuwa amesema angehudhuria sherehe hiyo. Rais mwingine mstaafu George HW Bush, 92, amesema hataweza kuhudhuria kutokana na umri wake. Bi Clinton amekuwa haonekani sana hadharani tangu aliposhindwa na Bw Trump uchaguzini Novemba. Wakati wa kampeni, Bw