Posts

Showing posts from January 29, 2018

Ikulu: Rais Magufuli Akutana na Maafisa Wakuu wa JWTZ

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini (CDF) Jenerali Venance Mabeyo kabla hajaanza kuwatambulisha Maafisa Wakuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (hawaonekani pichani) ambao wanatarajia kustaafu. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini (CDF) Jenerali Venance Mabeyo ambaye aliambatana na Maafisa Wakuu (sita) wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ambao wanatarajiwa kustaafu. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini (CDF) Jenerali Venance Mabeyo pamoja na Maafisa Wakuu (sita) wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wanaotarajiwa kustaafu ambao ni Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi wa Tanzania Luteni Jenerali James Mwakibolwa wanne kutoka (kulia), Meja Jenerali Michael...

Bunge kuunguruma kesho, wabunge watatu kuapishwa

Image
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linatarajiwa kuanza kunguruma kesho (Jumanne) na Mkoani Dodoma kwa kuanza kuapisha Wabunge wapya watatu pamoja na kupitisha miswada miwili ya sheria ambayo ilisomwa kwa mara ya kwanza katika mkutano wa tisa. Hayo yamewekwa wazi na taarifa rasmi iliyotolewa na ofisi za Bunge kupitia Kitengo cha Habari na Mawasiliano na kusema kuwataja wabunge hao ambao watakula kiapo cha uaminifu kuwa ni Mhe. Dkt. Damas Daniel Ndumbaro kutokea Songea Mjini, Mhe. Monko Justine Joseph wa Singida Kaskazini na kumaliziwa na Mhe. Dkt. Stephano Lemomo Kiruswa wa Longido. Aidha, katika mkutano huo wa 10 kutakuwa na wastani wa maswali 125 ya kawaida yanayotarajiwa kuulizwa na Wabunge huku wastani wa maswali 16 ya kiwa ya papo kwa hapo kuenda kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu ambayo yanatarajiwa kuulizwa siku ya Alhamisi mnamo februari mosi. Kwa upande mwingine, Kamati 16 za Bunge za kudumu ...

Lita 85 za Gongo zakamatwa Manyara

Image
Jeshi la Polisi mkoani Manyara limesema limekamata mitambo ya kutengenezea pombe haramu ya gongo pamoja na lita 85 za pombe hiyo, ambayo ni kinyume na sheria za nchi. Akizungumza na mwandishi wa www.eatv.tv Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara Agustino Senga, amesema vifaa hivyo pamoja na pombe imekamatwa kutokana na operesheni maalum inayoendeshwa na jeshi hilo. “Mkoa wetu wa Manyara umeendelea na misako mbali mbali ambapo tumekamata mitambo ya gongo pamoja na gongo huko mbulu, kijiji cha hydom Manyara, walimkata mtu mmoja Moshi Bula mwenye miaka 55, akiwa na mitambo minne ya kutengenezea mitambo ya gongo, hivi sasa yupo mahabusu na taratibu zikikamilika atafikishwa mahakamani,”, amesema Kamanda Senga. Kamanda Senga ameendelea kuelezea kwamba...Sambamba na hilo tumekamata lita 65 za pombe haramu ya moshi pamoja na watu watatu wanaohusika na pombe hiyo, ambao ni Neema Doto Matayo, mwenye miaka 21, Law...

Sumaye: wanaojiuzulu nafasi zao hawatambui majukumu yao

Image
picha ya mtandao Waziri Mkuu Mstaafu , Frederick Sumaye amefunguka na kusema kuwa kazi ya Mbunge ni kutetea wananchi wa jimbo lake na si kwenda kumsifia Rais na kudai wabunge waliojizulu nafasi zao kwa kigezo cha kumuunga mkono Rais hawakutambua majukumu yao. Sumaye amesema hayo kwenye kampeni za Ubunge wa marudio katika jimbo la Kinondoni zinazoendelea na kusema kuwa kwa Wabunge ambao wamejiuzulu nafasi zao na kwenda chama kingine kugombea tena hawafai kabisa kuwa wabunge kwa kuwa hawatambui maana ya Ubunge. "Kazi ya Mbunge si kwenda kumtetea Rais bali ni kutetea wananchi waliompa kura, kama Mtulia yeye anasema ameondoka na kudharau kura za watu wa Kinondoni kwa sababu amependezeshwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania basi akateuliwe na Rais kuwa Mbunge maana kazi yake ndiyo itakuwa kwenda kumtetea na kumsifia Rais. Watu ambao wanahama chama eti kwa sababu Rais ametenda mambo mema pamoja na ukweli kwamba mimi naweza kubishana sana maana hatujaona ...

Nabii Tito Apandishwa Mahakamani, Anyimwa Dhamana

Image
Onesmo Machibya almaarufu Nabii Tito aliyetengeneza vichwa vya habari kutokana na mahubiri yake ya kuhimiza ulevi na uasherati, amepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma, na kusomewa mashtaka ya kujaribu kujiua. Nabii Tito alifanya jaribio la kujiua Januari 25, mwaka huu akiwa mahabusu, ambapo inadaiwa kwamba alijikatakata na wembe kwa lengo la kuyakatisha maisha yake. Alipotakiwa kujibu mashtaka yanayomkabili, Nabii Tito awali alisema hakumbuki chochote kwa sababu yeye ni mgonjwa wa akili, lakini alipobanwa kwa mara nyingine, alisema ni kweli alitaka kujiua kwa sababu kuna sauti ndani ya kichwa chake iliyokuwa inamuelekeza kufanya kitendo hicho. Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Nabii Tito amerejeshwa rumande huku akiwekewa mapingamizi saba ya dhamana.

Matukio kwa Picha na Video Utambulisho wa Mbosso WCB

Image
WCB wakiwa katika picha ya pamoja, katikati ni msanii wao mpya, Mbosso. BURUDANI ya aina yake imepigwa na wasanii wa Lebo ya WCB usiku wa kuamikia leo wakati kumtambulisha msanii mpya katika kundi hilo, Mbosso ambaye awali alikuwa Yamoto Band kabla ya kundi hilo kuvunjika. Mbosso, Diamond na Rayvanny wakikamua. WCB ikiongozwa na Lejendari, Diamond Platnumz, wamemtambulisha huyo katika Ukumbi wa Hyatt Legency Hotel jijini dar es Salaam na kuhudhuriwa na mastaa kibao wakiwemo, Wema Sepetu na wengine pamoja na wanahabari. Diamond akimsalimia mama yake, Bi Sanura ukumbini hapo. WCB na mashabiki waki-enyoj event. WCB na mashabiki katika picha ya pamoja.   Diamond akikata mauno.

Dk Slaa, JPM wakutana kwa mara ya kwanza Ikulu

Image
Rais John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi mteule, Dk Willibrod Slaa, Ikulu Dar es Salaam. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Januari 29, mwaka 2018 na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa imesema Dk Slaa amemshukuru Rais kwa kumteua kuwa Balozi na kuahidi kuwa yupo tayari kutekeleza majukumu atakayopangiwa kwa kutanguliza maslahi ya Taifa. Imeeleza kuwa Dk Slaa ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa uongozi bora na kutekeleza mambo makubwa ikiwemo miradi ya ujenzi wa reli ya kisasa, ujenzi wa daraja la juu katika makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela, mradi wa uzalishaji umeme katika maporomoko ya mto rufiji na mapambano dhidi ya rushwa. “Kwa kweli naona faraja, ninafurahi Serikali ya Awamu ya Tano inatekeleza hatua kwa hatua karibu yote tuliyokuwa tunayapigania kwa miaka takribani 20 ya huko nyuma, mimi Dk Slaa nilikuwa napiga kelele kwa sababu nilikuwa naon...

Basi lateketea kwa moto Tanga Leo

Image
Basi la kampuni ya Tahmeed ambalo linafanya safari zake kutoka Dar es Salaam kwenda Mombasa Nairobi limeteketea moto katika kijiji cha Matumbi mkoani Tanga leo. Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga, Benedict Wakulyamba amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ya moto na kusema kuwa hakuna abiria ambaye amepata madhara na moto huo ulioteketeza basi hilo. "Ni kweli basi hilo limewaka moto leo, ila hakuna abiria aliyejeruhiwa wala kupata madhara yoyote kwa kuwa dereva alipoona dalili za moto alipaki gari pembeni na abiri ambao walikuwepo kwenye basi hilo kama 15 hivi wote waliweza kushuka mapema kabla ya moto kushika gari zima" alisema Wakulymba

Mtulia:nimefanya maamuzi ya Kiume

Image
Mgombea wa Jimbo la Kinondoni kupitia CCM, Maulid Said Mtulia amesema amefanya maamuzi ya kiume ya yeye kuhamia chama hicho kwa sasa kwa maana wapo wengi wanataka kufanya hivyo lakini wameshindwa kwa madai wanasubiri kulipwa kiunua mgongo. Mtulia ameeleza hayo wakati alipokuwa anaendelea kujinadi kwa wananchi wa jimbo la Kinondoni ambalo hapo awali alikuwa analishikilia yeye kupitia chama chake cha CUF kabla ya kujivua uanachama wake na kuenda kumuunga mkono Rais Magufuli katika jitihada zake za kuijenga nchi. "Kujiuzulu Ubunge sio mchezo, nimefanya maamuzi ya kiume maana kuna wenzangu wengine mpaka sasa hawawezi kutoka kwa sababu wanasubiri kiunua mgongo. Sasa kijana kama mimi nikae pale nisubirie kiunua mgongo hivi kweli ntaweza kuishi kwa kusubiri kiunua mgongo", alisema Mtulia. Aidha, Mtulia amesema amejinusuru kwa mengi kukihama chama chake cha awali ili aweze kuwapigania wananchi wa jimbo hilo kwa maana hapo awali alikuwa anashindwa...

DIAMOND PLATINUMZ AFUNGUKA KUMWALIKA WEMA SEPETU,AGUSIA PIA HAMISA MOBETTO,TUNDA NAYE AJAACHWA

Image
Majibu ya Diamond Platnumz Kuhusu Ujauzito wa Tunda HATIMAYE msanii kutoka industry ya Bongo Fleva, Diamond Platinumz ameamua kuanika ukweli kuhusu tetesi za kumpachika ujauzito Video Vixen wa Bongo, Tunda. Akifanya mahojiano maalum ya , Diamond amekanusha kumpachika mimba staa huyo na kudai kuwa hajawahi hata kutembea naye wala kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi.