Kwani ni lazima uolewe???
HAKIKA sifa na utukufu zimuendee yeye Jalali ambaye ametupa nafasi ya kuweza kukutana tena siku ya leo hii.Moja ya kitu kinachonishangaza kwa wanawake wengi ni kuwa na ndoto zaidi ya kuolewa kuliko kufikia ndoto zao halisi kwa maana ya maono ambayo wamekuwa wakiyawaza kwa muda mrefu. Tabia hii ya wanawake wengi ya kutaka au kukimbilia kuolewa si jambo baya, kama ikitokea ukapata bahati hiyo ya kuolewa lakini kama haitatokea sio ishu sana bali kumbuka kuwa kuna maisha nje ya kuolewa nayo si mengine ni maisha ya kufikia ndoto zako. Kama haujaolewa Ni kweli Mungu alituumba na kutuweka duniani ili tuujaze ulimwengu lakini hata hilo la upande wa pili nalo ni la kushukuru pindi linapokukuta, linauma ila kupunguza maumivu yake ni kulikuba li na kujifunza vitu vingine vingi ili uweze kuendelea na maisha mengine. Hulka ya wanawake kuolewa imekuwa ni sehemu ya wengi wao, utamsikia binti wa miaka 16 amemaliza darasa la saba anataka kuolewa eti kisa amefeli mtihani wa mwisho,