Posts

Showing posts from March 30, 2014

DK. MARIA KAMM AIBUKA KIDEDEA TUZO YA MWANAMKE BORA

Image
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewataka wanawake walioteuliwa kwenye Tuzo ya Mwanamke Bora wa mwaka 2013/2014 wasibweteke bali waendeleze juhudi zao na wazidi kung’ara zaidi. Ametoa wito huo jana usiku (Jumamosi, Machi 29, 2014) kwenye hafla ya kumtuza mwanamke bora wa mwaka 2013/2014 iliyofanyika kwenye ukumbi wa African Dream nje kidogo ya mji Dodoma. “Lazima muendelee kuonekana mnazidi kung’ara. Tuzo ni njema kwa upande mmoja lakini pia ina changamoto zake kubwa ikiwa ni ya kuendelea kubaki mnang’ara hadi waliowapigia kura wakawaona mnafaa,” alisema Waziri Mkuu. Utoaji wa tuzo hiyo uliwapambanisha Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka; Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Asha-Rose Migiro; Mwalimu Mkuu Mstaafu na Mbunge Mstaafu, Dk. Maria Kamm pamoja na Mbunge wa Same Mashariki, Bi. Anne Kilango Malecela. Kila mmoja alikabidihiwa Tuzo ya Mwanamke Bora na Waziri Mkuu Pinda lakini Dk. Maria Kamm ndiye aliyeibuka mshindi wa jumla kwa kukabidhiwa...

Mbeya City yainyuka Prisons, Mtibwa, JKT Ruvu kidedea

Image
Mbeya City Mtibwa Sugar iliyoitungua Coastal kwa mabao 3-1 BAO pekee lililofungwa katika dakika ya pili ya mchezo na Paul Nonga, lilitosha kuipa ushindi muhimu Mbeya City dhidi ya mahasimu wao Prisons na kuipumulia Yanga kisogoni kwenye mbio za kuwania nafasi mbili za juu za Ligi Kuu Tanzania bara msimu huu. Pambano hilo lililochezwakwenye uwanja wa Sokoine lilikuwa la vuta nikuvute, lakini ni Mbeya waliondeleza ubabe kwa wajelajela hao kwa kuwalaza kwa mara nyingine katika msimu wao wa kwanza wa ligi hiyo baada ya mchezo wa kwanza kuwanyuka 2-0. Kwa ushindi huo Mbeya City imefikisha pointi 45 moja pungufu na Yanga waliolala 2-1 Mkwakwani Tanga dhidi ya Mgambo JKT. Katika mechi nyingine ya ligi hiyo iliyochezwa uwanja wa Manungu, Mtibwa Sugar ilipata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya wageni wao Coastal Union. Mabao ya washindi katika mchezo huo yalifungwa na Jamal Mnyate dakika ya 14 kabla ya Coastal kusawazisha kupitia kwa Mbwana Hamis na Mussa Hassan kuipa uo...

LIGI KUU TANZANIA BARA :SIMBA YANGA ZACHAPWA

Image
Yanga yafa Mkwakwani, Azam yanusa ubingwa Yanga Azam KLABU Ya Azam imejiweka katika mazingira mazuri ya kutwaa taji la Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara ya kwanza baada ya jioni hii kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Simba, huku Yanga ikifa Mkwakwani. Yanga ilikumbana na kipigo cha mabao 2-1 toka kwa Mgambo JKT na kutoa nafasi kubwa kwa Azam kunyakua taji hilo kama itashinda mechi mbili kati ya tatu ilizosalia katika ligi kabla ya msimu kuisha. Mabao ya Mcha Khamis 'Vialli' na John Bocco 'Adebayor' kwa kila kipindi yalitosha kuiwezesha Azam kuendeleza rekodi ya kutopoteza mechi kwa msimu huu na kufikisha pointi 53. Bao la Simba lililokuwa la kusawazisha lilifungwa kwa kichwa na beki wake wa kati, Joseph Owino dakika chache kabla ya mapumziko. Nako jijini Tanga bao la mapema la mshambuliaji mkali, Fully Maganga na jingine la mkwaju wa penati wa Malimi Basungu lililotosha kuizamisha Yanga kwenye uwanja wa Mkwakwani, bila kutarajiw...

AJALI MBAYA YAUA WANAWAKE 12 MKOANI KILIMANJARO WALIOKUWA WAKIENDA MSIBANI....MAJINA YAO YATAJWA, SABA WAJERUHIWA

Image
Waombolezaji 12 waliokuwa njiani kuhani msiba wa mtoto aliyepoteza maisha baada ya kusombwa na mafuriko, wamefariki dunia na wengine saba wamejeruhiwa, baada ya gari lao kugongwa na malori mawili kwa wakati mmoja. Abiria hao walikuwa wanasafiri na gari dogo aina ya Toyota Pick Up namba T 170 AKZ kwenda kuhani msiba uliotokea katika kijiji cha Kongei kilichoko Hedaru mkoani Kilimanjaro. Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro , Robert Boaz waliofariki ni Stella John (45), Salma Kizoka (33), Marry Senzige (49), Neema Daniel (52), Rehema George, (29), Sophia Mbike (51), Ritta Kallani (55) na Kallan Stephano (55), Kolina Mmasa (55) na Bahati Daudi (25), Wengine ni Farida Kiondo (24) na Maria John (33) wote wakazi wa Kongei na kwamba miili yao imehifadhiwa katika hospitali ya Wilaya ya Same. Boaz aliwataja majeruhi kuwa ni Zubeda Mrindoko (42),Mipa Chediel (29) na Zubeda Mlita (32) ambao wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya KCMC kutokana na...

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA AWASILI MKOANI RUKWA LEO TAYARI KWA KUANZA ZIARA YAKE YA SIKU 21

Image
 Baadhi ya Wananchi na wanachama mbalimbali wakisubiri kumpokea katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana kabla ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege mjini Sumbawanga mkoani Rukwa mapema leo asubuhi.   Ndege iliyombeba Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana ikiwasili katika uwanja wa ndege mjini Sumbawanga,mkoani Rukwa mchana huu.   Ndugu Kinana akishuka kwenye ndege mara baada ya kuwasili mchana huu Sumbawanga mkoani Rukwa,tayari kwa kuanza ziara yake rasmi mkoni humu,ambapo ziara yake rasmi inaanzia Wilaya ya Nkasi,mkoani Rukwa.  Ndugu Kinana akipokelewa na viongozi mbalimbali wa CCM mkoa Rukwa mara baada ya kuwasili mapema leo mchana.  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akivalishwa skafu na vijana wa chipukizi mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege mjini Sumbawanga,mkoani Rukwa mapema mchana huu. Katikubu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na Kada maarufu wa CCM,Ndugu Chrisant Mzindakaya,mara baada ya kuwasili uwanj...

HABARI+PICHAZ..NI HATARIIIII MTAZAME HAMISA NA UTAALAMU WA KUCHEZA NA NYOKA..

Image
MREMBO aliyeng’ara kwenye Shindano la Miss Tanzania mwaka 2011, Hamisa Hassan ‘Mabeto’ amefunguka kuwa, licha ya baadhi ya wasichana wenzake kutokuwa na ujasiri wa kucheza na nyoka, yeye anao.   Mrembo aliyeng’ara kwenye Shindano la Miss Tanzania mwaka 2011, Hamisa Hassan ‘Mabeto’   Akipiga stori na Ijumaa, Mabeto alisema awali alikuwa muoga lakini taratibu alianza kumzoea kiumbe huyo na sasa humtumia hata katika shughuli zake za kimodo anazofanya.   “Hizo picha nilikuwa kwenye ‘photo shooting’ (upigaji wa picha) ila kiukweli nina utaalam wa kucheza na nyoka, unajua siyo kila mtu anao ujasiri wa kumchezea, kwanza anatisha ila mimi nilianza kumzoea taratibu,” alisema Mabeto.

MAUHAJI YA KUTISHA YA MTOTO YAFANYIKA UKO MKOANI MANYARA WILAYA YA MBULU.

Image
Pata kisa hiki cha kusikitisha ambacho kilikuwa hakijawahi tokea katika kijiji hiki kwani kilisababisha vilio kutanda ndani ya mji mzima.  Jeneza la marehemu Jenefrida likiwa limebebwa na waombolezaji kuelekea makaburi MAHUAJI. Mahuaji haya yalitokea mnamo tarehe 25/03/2014 katika kijiji cha GIDEMOSA kata ya DONGOBESH wilaya ya MBULU mkoani Manyara mnamo majira ya saa tisa alasiri ambapo mtoto JENIFRIDA PAULO aliweza kuuwawa Kikatili kwa kuchomwa kisu pemebezoni ya kichwa na hatimaye kuchinjwa shingo na uku kolomea likiwa limening'inia na akisaidiwa kushikiliwa na ngozi tu.. CHANZO CHA KIFO. Marehemu JENIFRIDA PAULO mnamo trh 25 kabla ya kukumbwa na mauti hayo akiwa nyumbani kwao mchana, akiwa yeye na mama yake mzazi. Mama wa marehemu akiwa ndani ya nyumba kubwa kapumzika kutokana na matatizo ya kiafya yanayomkaribi kwa muda, ilamuagiza mwanae(marehemu) aende katika nyumba ndogo yaani jiko na stoo akatoe kuni zilizokuwa nje ya myumba na akaziweke ndani ili usiku waw...

JE WAJUA KUA NGUO ZA NDANI HUCHANGIA, UGUMBA? SOMA MAKALA HII UJUE MENGI

Image
TAFITI Za Kisayansi Zimebaini Kuwa Nguo Za Ndani Hasa Zinazobana Kwa Wanaume Na Zile   Za Aina Ya Nailoni (Nylon) Zinaathiri Uwezo Wa Mbegu Za Kiume, Hivyo Kushindwa Kutunga Mimba. Utafiti huo uliofanyika katika nchi za Ufaransa na Uingereza na kuchapishwa katika Gazeti la Daily Mail la Uingereza unabainisha kuwa, wanaume wanaovaa nguo za ndani zinazobana na zile zilizotengezwa kwa malighafi ya nailoni, mbegu zao za kiume (manii) huwa nyepesi na kupoteza uwezo wa kutunga mimba Vazi la ndani la wanaume linalojulikana kama boksa na nguo nyingine za ndani za kubana zenye asili ya nailoni, zinakuwa na athari kubwa zaidi hasa zinapovaliwa katika sehemu zenye joto, kama Dar es Salaam. Kutokana na matokeo hayo, wanasayansi wameonya kuwa wanaume wanapaswa kuchukua tahadhari, hasa kutokana na tafiti nyingi za karibuni kuthibitisha kuongezeka kwa matatizo ya mbegu za kukosa uwezo wa kutunga ujauzito katika nyumba ya uzazi ya mwanamke. Akizungumzia utaf...

MKE WA MTU AFUMANIWA NA MWANAUME MWINGINE.....WAPEWA KICHAPO WALAZIMISHWA KUFANYA MAPENZI HADHARANI.

Image
    Hii ajali imetokea huko Anambra State Nigeria baada ya Mke wa mtu kukamatwa na mumewe live akifanya mapenzi na bwana wake wa pembeni. Watu wakaona isiwe tabu wakachukua sheria mkononi na kuwalazimisha waendelee kufanya  mapenzi mbele ya umati wa watu. Wakati yote hayo yanaendelea mwenye mke hakutaka kabisa kushuhudia badala yakealienda nyumbani kumfungia mke wake virago. Haya majanga yalitokea karibu kabisa na Chuo kikuu cha Anambra State. Kazi kwenu mnaotoka na wake za watu mtakamatwa na kulazimishwa mfanye mapenzi hadharani kama sio kugandana.