Posts

Showing posts from February 14, 2018

Katibu wa Bunge Azungumzia Afya ya Spika Job Ndugai

Image
Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai amesema hali ya afya ya Spika wa Bunge, Job Ndugai aliyepo nchini India inaendelea vizuri. Kagaigai amesema leo Februari 14,2018 kuwa Spika Ndugai yupo India kwa ajili ya kuangalia afya yake (check-up) na anatarajiwa kurejea nchini wakati wowote. Katibu huyo wa Bunge amesema, “Tulikwisha kusema kwamba Spika yuko India kwa ajili ya ‘check-up’ na hali yake inaendelea vizuri.” Alipoulizwa kuwa Spika atakuwa ughaibuni hadi lini, Kagaigai amesema: “Hilo ni kati ya daktari wake na yeye lakini ninachoweza kusema wakati wowote anaweza kurudi nchini.”

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MAKAMU MKUU WA CHUO KIKUU CHA BAGAMOYO IKULU

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo(University of Bagamoyo UB) Profesa Costa Mahalu mara baada ya kufanya nae mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo(University of Bagamoyo UB) Profesa Costa Mahalu mara baada ya kufanya nae mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni mtoto wa Profesa Mahalu ambaye ni Mwanasheria wa Kijitegemea Jaja Costa Mahalu. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mtoto wa Profesa Mahalu ambaye ni Mwanasheria wa Kijitegemea Jaja Costa Mahalu mara baada ya kumaliza mazungumzo na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo(University of Bagamoyo UB) Profesa Costa Mahalu Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

Mama Diamond Ajitoa Kwa Zari, Mobeto

Image
DAR ES SALAAM: Mama mzazi wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kassim (pichani) amejitoa kwenye gogoro linaloendelea kati ya ‘wakweze’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ na Hamisa Mobeto. Kabla ya kauli ya mama Diamond juu ya warembo hao mapema wiki hii, wikiendi iliyopita kuliibuka ubuyu kwenye mitandao ya kijamii hasa Instagram kuwa, ugomvi kati ya Zari na Mobeto ulikuwa umeibuka upya baada ya kupoa kwa siku kadhaa. Uchunguzi wa Risasi Mchanganyiko ulibaini kwamba, ugomvi baina ya wawili hao ulirejea upya baada ya Mobeto kukutana na Diamond kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu katika Kitengo cha Ustawi wa Jamii na kukubaliana juu ya malezi ya mtoto wao, Abdulatif Nasibu ‘Prince Dully’. Ilisemekana kwamba, kuna maneno aliyoweka Zari kwenye Mtandao wa Snapchat yakiashiria kutokuwepo kwa maelewano kati yake na Diamond kufuatia tukio hilo lililoonekana kumweka jamaa huyo karibu na Mobeto. Kama hiyo haitoshi, kuna ubuyu kuwa...

Rais Magufuli ashiriki Misa ya majivu

Image
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameungana na waumini wa Kanisa Katoliki na wakristo wengine katika ibada ya Jumatano ya majivu inaoashiria kuanza kwa mfungo mtukufu wa kwaresma. Magufuli akiwa na mkewe, Mama Janeth Magufuli wameungana na waumini hao katika ibada iliyoongozwa na Muadhama Askofu Mkuu, Polycarp Kardinali Pengo wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Dar, leo Februari 14, 2018.

Rais Magufuli Ateua Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Mpya

Image
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 14 Februari, 2018 amemteua Meja Jenerali Yakubu Hassan Mohamed kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). Pamoja na uteuzi huo, Mhe. Rais Magufuli amempandisha cheo kutoka Meja Jenerali na kuwa Luteni Jenerali. Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed anachukua nafasi ya Luteni Jenerali James Alois Mwakibolwa ambaye amestaafu.

LULU AKIWA GEREZANI MIEZI 3 SASA,MAPYA TENA YAANIKWA,MAMA YAKE ANENA

Image
Ikiwa takribani miezi 3 sasa, tunaambiwa Lulu amenenepa huko gerezani kwa kukubaliana na hali halisi na hajawahi kuumwa. Afisa mmoja wa magereza akichonga na globalpublishers amesema Lulu ndie amegeuka kuwafariji wanaoenda kumtembelea hasa ndugu zake badala ya wao kumfariji. Lulu amekuwa akiwaambia wasijisikie vibaya hakuna aijuaye Kesho yake na yeye wachukulie Kama yupo shule Ya Boarding kuna siku atakuwa Huru . Munalove aliyeanzia kuigiza Kaole ambaye amekuwa na Lulu kwa mvua na jua kwa Miaka mingi sasa ambapo hakosi kwenda gerezani kumuona lulu Kila wiki, alipoulizwa na GPL alisema . . “anatushangaza hata sisi, kwanza kanenepa na anaonekana mwenye furaha maana wakati mwingine tukienda kumuona tunakuwa na simanzi lakini yeye anakuwa mfariji wetu akisema kwamba ipo siku atatoka na kuwa huru tena,” . . Mama Lulu yeye alipopigiwa simu na GPL aliwaka kwa kuja juu akisema hataki kabisa kusikia magazeti wala waandishi wa habari kwakuwa yeye sio superstar, ameomba Lulu ...

Kiongozi CHADEMA Auawa, Mbowe Asimulia Alivyotekwa, Mwili Wake Waokotwa Ufukweni

Image
  MWENYEKITI wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kiongozi wa chama hicho katika Kata ya Hananasif, Daniel John amefariki dunia katika mazingira ya kutatanisha. Akizungumza na waandishi wa habari jana Februari 13, 2018, Mbowe alisema John alitoweka siku moja iliyopita. Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema hana taarifa hizo lakini anawasiliana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni.   Amesema baada ya mawasiliano atatoa ufafanuzi leo  Februari 14,2018. Mbowe alisema John ambaye ni katibu kata alitoweka akiwa na Reginald Mallya ambaye alijikuta yupo ufukweni mwa bahari. Mbowe alisema walitoa taarifa polisi kuhusu kutoweka kwa John na kwamba, walipokwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) walielezwa kuna mwili ulipelekwa na polisi. Alisema mwili huo ulitambuliwa na mkewe John na una michubuko inayoashiria alikabwa, una jeraha la panga kichwani na upande mmoja wa kichwa umebonyea kuashiria alipigwa na kitu ...