Mzee Akilimali aliamsha dude Yanga
Katibu wa Baraza la Wazee wa Klabu ya Yanga, Ibrahimu Akilimali amemtaka Makamu Mwenyekiti wa Klabu hiyo Clement Sanga kujiuzulu kwa madai kuwa yeye ndiye chanzo cha matatizo yote yanayotokea ndani ya Klabu hiyo. Mzee Akilimali amesema wamegundua mgomo uliotokea hapo jana kwa wachezaji kutohudhuria mazoezi ni njama iliyopangwa na Sanga wakidai kuwa wachezaji hawajalipwa mishahara yao suala ambalo sio sawa. "Mimi naona tu kwamba Sanga sasa imefikia hapa, ili tufanye vizuri nawasihi Watanzania wote hususani wana Yanga na wapenzi wa Yanga bwana Sanga sasa hivi atamke kujiuzulu, chonde chonde Bwana Sanga iache Yanga watu tuketi pamoja na wewe mwenyewe tuchague viongozi Yanga tusonge mbele" amesema Mzee Akilimali Mzee Akilimali amesema siku moja kabla ya mazoezi alionekana Makamu Mwenyekiti wa Klabu hiyo Sanga akiwa na Nahodha wa Timu hiyo Nadir Haroub 'Canavaro' pamoja na Mshambuliaji wa Kimataifa Thaban Kamusoko ambapo baada ya kutoka hap...