Posts

Showing posts from December 23, 2013

ANGALIA PICHA ZA VURUGU ZA WAFUGAJI NA WAKULIMA YALIOTOKEA MALINYI ULANGA

Image
 Kituo cha Polisi Kilichovamiwa na wananchi ambapo Walifanya uharibifu mkubwa wa mali pamoja na kuchoma moto gari moja lilokuwa kituoni hapoa na katika vurugu hizo  watu watau walifariki dunia   Picha ya mmoja wa marehemu kutokana na Vurugu za wafugaji na wakulima ambapo wananchi walitaka kuvamia kituo cha polisi malinyi.Katika vurugu hizo watu watatu walipoteza maisha.CHANZO  MATUKIO BLOG

MCHAWI AKAMATWA DAR NA KUUAWA LIVE BAADA YA KUDONDOKA NA UNGO

Image
WANANCHI wenye hasira kali wamempiga hadi kumuua mtu mmoja mwanaume aliyesadikiwa kuwa ni mchawi baada ya kuanguka akiwa amepanda ungo maeneo ya Mbezi Luis jijini Dar es Salaam, Mtanzania limeshuhudia. Kijana huyo mkazi wa Mwanza anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 20 hadi 25, alianguka jana saa 12 asubuhi maeneo hayo baada ya kudai kuwa alikuwa kwenye safari zake za kishirikina. Kabla ya kufariki alisema “mimi nilikuwa na wenzangu sita, wanaume watatu na wanawake watatu ambapo tulikuwa tunatoka Mwanza kuelekea kwenye mkutano wetu” “Lakini mimi kwa bahati mbaya nilikiuka masharti tuliyopewa na mkuu kwa kufungua macho ndipo ghafla nilianguka na kupata kadhia hii inayopelekea mauti yangu” Hata hivyo kutokana na vurugu zilizokuwapo eneo hilo la tukio, ambapo wananchi wa eneo hilo walikuwa wanataka kumuua, kijana huyo alishindwa hata kutaja jina lake kutokana na kipigo alichokuwa anakipata kutoka kwao. Kwa mujibu ...

MCHAWI AANGUKA PEMBENI YA KANISA AKIWA NA KIGANJA CHA MKONO WA MTU MDOMONI.

Image
  Dada mmoja aliye julikana baadae kama Esther alianguka pembeni ya kanisa huko Naija huku akiwa na kiganja cha mkono wa mtu mdomoni na  gongo kubwa mkononi, baada ya kuhojiwa baadae alisema kwamba yeye alikuwa kwenye safari zake tu na baadae kujikuta amepoteza fahamu eneo hilo.

YANGA YAMTEMA RASMI BRANDTS, BIN KLEB AWEKA MAMBO HADHARANI LEO JANGWANI!!

Image
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano Abdallah Bin Kleb (katikati) akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga, kushoto ni Musa Katabaro na kulia Afisa Habari Baraka Kiziuguto. Picha kwa Hisani ya Young Africans Official Website Na Baraka Mpenja KIMENUKA jangwani!. Siku mbili tu baada ya Yanga kupata kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Simba SC katika mechi ya Nani Mtani Jembe, uongozi wa klabu hiyo umetangaza kuachana na kocha wake, Mholanzi, Ernie Brandts. Mwenyekiti  wa Kamati ya Mashindano wa klabu ya Yanga Abdallah Bin Kleb amesema Uongozi umempatia taarifa (Notice) ya siku  thelathini (30) , Brandts juu ya kusitisha mkataba wake kuanzia jana Disemba 22 mwaka huu. Bin Kleb amesema maamuzi hayo yanafuatia muenendo wa matokeo mabaya katika michezo iliyopita ya Ligi Kuu, kirafiki na bonanza la Nani Mtani Jembe dhidi ya Simba SC mwishoni mwa wiki. “Hatua ya Yanga kusitisha mkataba  na Brandts isichukuliwe kama chuki bali ni moja y...

MAFUFU NA H.BABA NDANI YA BIFU ZITO

Image
LILE bifu lililopo kati ya msanii wa muziki na filamu, Hamis Ramadhani ‘H.Baba’ na Jimmy Mafufu limezidi kushika kasi ambapo Mafufu ameapa kutozungumza na H. Baba milele. H. Baba. Akistorisha na gazeti hili Jimmy alisema anamshangaa H.Baba kusema kuwa anatafuta umaarufu kupitia jina lake jambo ambalo siyo kwani yeye ni maarufu tangu zamani na hawezi kupata umaarufu kupitia kwa mkata viuno. Mafufu. “Siwezi kuongea na H.Baba mpaka naingia kaburini kwa sababu ana maneno sana na anapenda sana bifu na kila mtu, kwanza yeye ndiye anayetafuta umaarufu maana hivi karibuni tu alikuwa akizozana na Diamond na huko nyuma aliwahi kuwa na bifu na  Uwoya sasa mimi siyo mtu wa kujibishana naye kihivyo,”alisema Jimmy.

MASTAA 10 VINARA WA SKENDO 2013 HAWA HAPA

Image
KATIKA ulimwengu wa mastaa kuna ambao wamekuwa wakitikisa kwa skendo mbalimbali kwa mwaka 2013 ambazo ziliwachefua mashabiki wao, Ijumaa Wikienda linakupa Top 10 ya skendo hizo. AGNES GERALD ‘MASOGANGE’ Video Queen huyo alitikisa mwaka 2013 kwa skendo ya kukamatwa na dawa za kulevya huko Afrika Kusini na kuwekwa rumande kwa siku kadhaa. Baadaye alifikishwa mahakamani ambapo iligundulika kuwa mzigo aliokuwa amebeba siyo dawa za kulevya ila ni unga unaotumika kama dawa za binadamu na kesi ikaishia hapo. Pia Masongange alikuwa kinara wa kupiga picha za nusu utupu ambazo alizitundika mtandaoni na kugeuka gumzo kubwa. WEMA SEPETU Wema alitikisa kwa ishu ya kurudiana na mwanamuziki wa kizazi kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ikiwa ni baada ya kukutana nchini China na kupiga picha za kimahaba, hali iliyozua gumzo kila kona na mitandaoni. Wema alirudiana na Diamond huku akijua kwamba mwanamuziki huyo alikuwa na mpenzi mwingine ambaye ni mtangazaji wa DTV, Penniel Mungilwa ...

HUYU DEMU SIMWELEWI, ETI ANATAKA NIMPIGE PICHA AKIWA MTUPU

Image
SISI ni majirani tumetokea kuzoeana tu kidogo kwakuwa mwenzangu yeye ni mwenyeji mimi nimemkuta tu hapo nilivyo hamia,  lakini naona kama kuna mazoea fulani ya ajabu, hii ni mara ya tatu huyu dada ananiomba nimpige picha tena akiwa amevaa kiajabu ajabu,  siku nyingine anadiriki hata kunigongea chumbani kwangu ili nitoke tu nimpige picha halafu aendelee na shughuli zake. sasa imekuwa kero Simuelewe kabisaaaa.  Tena kibaya zaidi jana saa tatu usiku kaniita chumbani kwake eti nimpige picha na kiguo chake kama mnavyoona hapo pichani yani tabu tupu. NIPE MAONI YAKO NDUGU MDAU WETU, NA USISAHAU KULIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK

meza ya magazeti leo jumatatu

Image

SHILOLE ALIZWA MCHANA KWEUPEEEE

Image
MSANII wa filamu na muziki Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ hivi karibuni alimwaga machozi hadharani baada ya kuibiwa simu yake ya mkononi, Mwananyamala jijini Dar es Salaam. Zuwena Mohamed ‘Shilole’. Kwa mujibu wa ‘sosi’ wetu aliyemshuhudia mwanadada huyo akilia, tukio hilo lilitokea Jumapili baada ya Shilole kushuka kwenye gari lake na kumwachia fundi kwa ajili ya marekebisho ambapo alipanda teksi na kuelekea saluni, alipofika akajikuta hana simu. “Shilole alilia kama mtoto mdogo kwani alikuwa anatakiwa kusafiri siku hiyohiyo usiku kwenda Uingereza, ikabidi aanze kufanya jitihada za kupata simu nyingine lakini kwa kuwa ilikuwa ni wikiendi, kazi ilikuwa ngumu kwake,” kilisema chanzo hicho. Mwandishi wetu alipojaribu kumtafuta Shilole ili aeleze simu ilikuwa ya gharama kiasi gani, hakuwa akipatikana hewani mpaka gazeti hili linaenda mtamboni.

WASHAURI KUWA RAIS KIKWETE AUNDE SUK

Image
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akifungua mkutano wa Baraza Kuu la Uongozi la CUF huko Buguruni, kulia ni Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Hamad Masoud Khamis Haji OMKR — Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amesema nchi inakumbwa na msukosuko mkubwa wa kiuongozi na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Jakaya Kikwete anapaswa kuchukua maamuzi ya busara ya kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa hivi sasa, ili kulinusuru Taifa. Profesa Lipumba amesema hayo leo (21/12/2013) wakati alipokuwa akifungua mkutano wa Kawaida wa Baraza Kuu la Uongozi la CUF, unaofanyika Makao Makuu ya chama hicho Buguruni, Dar es Salaam.Amesema msukosuko huo unaonekana wazi kufuatia taarifa ya Ripoti ya Kamati ya Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira, Hali ya kukosekana kwa uwazi katika Mchakato wa katiba na Hatma ya Uchaguzi Mkuu 2015, pamoja na malalamiko ndani ya CCM kwamba kuna Mawaziri wengi ndani ya Serikali ni mizigo. ...

MUME WA MTU AMLIZA KAJALA LIVE

Image
BAADA ya kuzagaa kwa skandali kuwa mwigizaji Kajala Masanja anatembea na mume wa mtu, staa huyo ameibuka na kueleza kulizwa na ishu hiyo akianika siri nzito ambayo ilikuwa nyuma ya pazia. Kajala Masanja. Taarifa za awali ambazo Ijumaa Wikienda lilizipata zilieleza kuwa tangu habari hiyo ya mjini ilipuke kama moto wa kifuu kwenye mitandao na baadhi ya magazeti (siyo ya Global), Kajala amekuwa akiishi katika hali ya masikitiko kwani suala hilo limemtesa moyoni. Kikizungumza na paparazi wetu, chanzo makini kilicho karibu na staa huyo kilisema kuwa Kajala amekuwa kwenye mateso juu ya skendo hiyo kwani haina ukweli na aliumia zaidi kuona inazidi kubebewa bango kila kukicha na wabaya wake. “Kajala anazungumza waziwazi kuwa hakuna kitu kinachomtesa kwa sasa kama suala hilo. Kajala. “Yupo tayari kufunguka ukweli juu ya jambo hilo kwani haoni sababu ya kuumia katika jambo ambalo halina ukweli. “Kwanza huyo Mwasha (Shamim) anayedaiwa kuwa anaibiwa bwana na Kajala ni...

LULU NI HATARI SANA KWA MISAMBA

Image
Hatari Sana..! We mutoto we..! Chunga usifunjike!