Posts

Showing posts from July 24, 2017

Ruby Ajazwa Kibendi

Image
Msanii Hellen George ‘Ruby’ JAZA ujazwe! Habari ya mjini kwa sasa inamhusu sexy lady wa Bongo Fleva, Hellen George ‘Ruby’ kujazwa kibendi na staa mkubwa wa muziki huo, licha ya kwamba mwanadada huyo amekuwa akifanya siri. Chanzo makini kililieleza Ijumaa Wikienda kuwa, Ruby ana ujauzito ambao umekuwa ukimfanya ajifichefiche huku akimficha aliyemjaza kibendi hicho kwa madai kuwa, jamaa aliyempachika kibendi amezaa na wanawake tofauti. Kama ilivyo desturi yake, Ijumaa Wikienda lilimnyatia Ruby ambaye alikiri kuwa mjamzito, lakini akatia ngumu kumtaja baba kijacho na umri wa mimba yake kwani wakati muafaka haujafika. “Mimba bado ni changa, siwezi kusema ina miezi mingapi. Kuhusu nimepewa na mwanamuziki mkubwa, siyo kweli ila ipo siku wakati ukifika nitasema ni ya nani,” alisema Ruby

MUIGIZAJI WA HOME ALONE AFARIKI DUNIA

Image
Aliyekuwa muigizaji wa Home Alone1,Home Alone 2 na Lost in New York, John Heard ameripotiwa kufariki dunia akiwa katika chumba cha hoteli moja jijini Callifonia. Muigizaji huyo ambaye amepata umaarufu kupitia filamu hizo zilizotamba miaka ya 90, amefariki akiwa na miaka 72, Mpaka sasa chanzo cha kifo cha muigizaji huyo hakijawekwa bayana. Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, marehemeu alikuwa amejipumzisha katika hoteli hiyo baada ya kufanyiwa upasuaji siku ya Jumatano katika kituo cha afya cha Stanford. Marehemu ameacha mke Margot Kidder na mtoto wake mmoja aitwaye John Matthew “Jack”

Uwoya, Kelvina Hapatoshi!

Image
Irene Uwoya. SIFA ya ubuyu wenye rangi nyekundu ni kuacha rangi midomoni vivyo hivyo penzi ni kikohozi kulificha huwezi! Wamama wawili wa Bongo Muvi, Irene Uwoya na Kelvina John, wanadaiwa kuingia kwenye vita nzito ya penzi la msanii wa Bongo Fleva, Patrick Chrisopher ‘PCK’ na sasa hapatoshi, ni Ijumaa Wikienda pekee lenye ubavu wa kukupa ubuyu ulionyooka. MAPENZI SHATASHATA Chanzo makini cha ubuyu huo kililieleza Ijumaa Wikienda kuwa, kwa sasa PCK na Kelvina ni mahaba niue au mapenzi shatashata, jambo ambalo linamchukiza Uwoya ambaye anasemekana kwamba, aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume huyo anayesifika kwa kuwachanganya na kuwapanga kama mafungu ya nyanya mastaa wa kike Bongo. “Hivi watu wa ubuyu mnajua kuwa kuna vita nzito kati ya Uwoya na Kelvina? Unaambiwa sasa hivi vita yao siyo ya nchi hii na wanaviziana kama Korea Kaskazini na Marekani, eti, kisa nasikia wanagombea penzi la PCK. WAKUTANA BAA YA UWOYA “Tukio bichi la Uwoya na Kelvin

Lipumba Atangaza Kuwavua Uanachama Wabunge 8 wa CUF

Image
Profesa Ibrahim Lipumba. Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama cha Wananchi (CUF) limewavua uanachama wabunge wanane wa chama hicho kwa madai ya utovu wa nidhamu, yakiwemo kukisaliti chama hicho. Mwenyekiti wa CUF, anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba amesema, baraza pia limewavua uanachama madiwani wawili wa viti maalumu mkoani Dar es Salaam, kwa makosa kama hayo. Profesa Lipumba ametangaza uamuzi huo leo Jumatatu, Julai 24 wakati wa mkutano na wanahabari uliofanyika makao makuu ya CUF, Buguruni, Dar es Salaam. “Leo asubuhi tumewasilisha nyaraka  za hatua hizi kwa Spika na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa hatua zaidi,” amesema Profesa Lipumba. Amesema wabunge hao wanane ni kati ya 10 walioitwa hivi karibuni na Kamati ya Maadili na Nidhamu kwa mahojiano wakitakiwa kujibu tuhuma zinazowakabili za kukihujumu chama hicho kwa maelezo kuwa walitaka kushirikiana na Chadema kumwondoa yeye madarakani.

WAZIRI PROF. MAGHEMBE AMEWAPOKEA MABILIONEA 28 KUTOKA MABARA YOTE DUNIANI KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI

Image
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na Mabilionea 26 kutoka taasisi ya Young Presidents Organisation (YPO) wakiwa na wenza wao katika moja ya hoteli ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakati wa mapokezi yao jana kwa ajili ya ziara yao ya siku tatu nchini Tanzania. Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Alan Kijazi (katikati waliosimama) akizungumza na Mabilionea hao. Kulia kwake ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe . Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na Mabilionea hao jana katika moja ya hoteli ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Alan Kijazi. Kiongozi wa msafara wa Mabilionea hao, Perry Amber akizungumza wakati wa mapokezi hayo jana katika moja ya hoteli ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.  Mabilionea hao kutoka taasisi ya Young Presidents Organ

Mboto: Mzee Majuto Hajafa Jamani!

Image
MSANII wa filamu nchini, Haji Salum maarufu kama Mboto , amekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni zinazodai kuwa nguli wa vichekesho katika tasnia ya uigizaji , Amri Athuman maarufu kama King Majuto amefariki dunia. Mboto baada ya kupata taarifa hizi alifunga safari kuelekea mkoani Tanga ambapo ni nyumbani kwa Mzee Majuto na kumkuta hai, na amekanusha uvumi huo kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuposti picha inayowaonyesha yeye na Majuto wakiwa nyumbani kwake, na picha hiyo iliambatana na maneno yafuatayo: “ Baada ya kupata taarifa mbaya kuhusu Mzee Majuto nimelazimika kuja kwake Tanga . Ni kweli anaumwa ila anaendelea vizuri na si kama watu walivyozusha kuwa mzee hatunaye. Kwa sasa mzee ni mzima nipo naye Tanga ,” ameandika Mboto . Siku chache zilizopita, gazeti la Ijumaa Wikienda liliripoti taarifa za kuumwa kwa Mzee Majuto , anayesumbuliwa na tatizo la ngiri, lakini jana kwenye mitandao ya kijamii zikaenea taarifa zisizo za kweli kwamba King Majuto amefariki