Posts

Showing posts from July 21, 2017

Hatimaye Millen Magese Apata Mtoto Baada ya Upasuaji Mara 13

Image
Happiness Millen Magese akiwa amekumbatia kichanga chake.   Miss Tanzania mwaka 2001, Happiness Millen Magese ambaye anafanya kazi ya uwanamitindo amebahatika kupata mtoto wake wa kwanza Julai 13 mwaka huu.   Millen amewahi kumwaga machozi hadharani akielezea mateso yanayotokana na tatizo aliloligundua kwake toka akiwa na umri wa miaka 13 la mirija yake kuziba mwaka 2007.   Kuna kipindi alikata tamaa mpaka akajiandaa kuondoa kizazi na hapo ni baada ya kufanyiwa  oparesheni zisizopungua 13 ambapo pamoja na hayo, aliambiwa moja ya tiba ya tatizo hilo liitwalo ‘Endometriosis’ kwa kizungu, ni kuzaa.   Baada ya mateso yote usiku na mchana pamoja na kutumia gharama kubwa kwenye matibabu South Africa na Marekani, hatimaye amefanikiwa kupata mtoto wa kiume July 13, 2017 Hospitalini New York Marekani na anaitwa Prince Kairo Michael Magese.   Millen ameeleza namna alivyoteseka huku akimshukuru Mungu kwa muujiza huo wa aina yak...

Picha za Mazishi ya Mama Zari, Uganda

Image
Mama Diamond (wa tatu kushoto) akiwa na mkwe wake, Zari (kushoto kwake). Waombolezaji wakiswali msibani. Mama mzazi wa Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ , Halima Hassan aliyefariki dunia jana asubuhi, baada ya kuugua kwa wiki kadhaa na kulazwa hospitali amezikwa leo Julai 21, 2017 katika Kitongoji cha Munyonyo, Kampala. Kina mama wakiomboleza. Alhamisi iliyopita Gazeti la Amani liliripoti hali ya ugonjwa ya mama huyo kutokuwa nzuri baada ya kudaiwa kupumulia mashine ya oksijeni kwenye Kitengo cha Wagonjwa Mahututi (ICU) katika Hospitali ya Nakasero iliyopo nchini Uganda akisumbuliwa na maradhi ya moyo na figo ambayo yamekuwa yakimsumbua tangu kufariki kwa mkwe wake, Ivan Ssemwanga .   Hali ilivyokuwa nyumbani kwa mama Zari. Kwa mujibu wa chanzo ndani ya familia hiyo, mama Zari alipata matatizo ya moyo na figo baada ya kuanguka ghafla na kichwa chake kujigonga, hali iliyosababisha akimbizwe hospitalini haraka. Kaburi ambamo mwili wa marehem...

ALICHOANDIKA DIAMOND PLATNUMZ KUHUSU KIFO CHA MAMA YAKE ZARI THE BOSS LADY

Image
Msanii wa Bongo Fleva  Diamond Platnumz  ametumia IG Yake kuweka ujumbe huu kuhusu Kifo cha mama yake  ZARI   ambaye ni mama watoto wawili wa Diamond Platnumz. Diamond PlatnumzMwenyez Mungu ailaze Roho yako Mahali Pema Peponi Amini. Mama mzazi wa Zari amefariki  Asubuhi ya July 20 2017.

Tundu Lissu agoma Kupimwa mkojo

Image
Tundu Lissu(Mb) amekataa kupimwa mkojo baada ya kufikishwa kwa Mkemia   Asema kipimo hicho hakihusiani na tuhuma za uchochezi Taarifa za awali ziliarifu kuwa, Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema baada ya Tundu Lissu kutolewa Kituo cha Polisi cha Kati leo mchana, amefikishwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali na kupimwa mkojo. Mapema asubuhi, mawakili akiwamo Fatma Karume walizuiliwa kuonana naye huku Jeshi la Polisi likisema litaendelea kumshikilia hadi uchunguzi utakapokamilika. Mbunge huyo wa Singida Mashariki amekamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), akielekea Kigali, Rwanda kwenye kikao cha Halmashauri ya EALS kilichoanza jana. "Kabla ya kuelekea nyumbani kwake Tegeta, wamempeleka kwa mkemia mkuu na ameshapimwa mkojo, sasa sijui ni kitu gani wanachunguza, kwa sasa wameshaelekea nyumbani kwake kwa ajili ya kumpekua,"amesema Mrema. Licha ya kulala rumande hakuna aliyeruhusiwa k...

Siku ya Mashujaa Kufanyika nchini kote kwa huduma za kiafya

Image
Meja Jenerali Simon Mumwi ambaye ni Mkuu wa Mipango na Maendeleo wa JWTZ akizungumza na Waandishi wa habari. JESHI la Ulinzi laWananchi wa Tanzania leo limetoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya maadhimisho ya Siku ya Mashujaa yanayotarajiwa kufanyika Julai 25 mwaka huu. Maadhimisho hayo kama ilivyo desturi ya nchi hutoa fursa ya kuwakumbuka mashujaa wa Tanzania waliotoa maisha yao kwa ajili ya kupigania nchi yetu.  

MH. RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AWASILI KIGOMA AKITOKEA KAGERA, AZINDUA MIRADI YA MAENDELEO NA KUHUTUBIA WANANCHI KWENYE MIKUTANO YA HADHARA AKIWA NJIANI

Image
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Kakonko kabla ya kuzindua Ujenzi wa barabara ya Kibondo -Nyakanazi yenye urefu wa kilometa 54,katika mkoa wa Kigoma Rais yupo mkoani Kigoma kwa Ziara ya siku Tatu Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikazia jambo wakati akiwahutubia wananchi wa Kakonko Kibondo katika mkoa wa Kigoma Rais yupo mkoani Kigoma kwa Ziara ya siku Tatu Wananchi wa Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma wakisikiliza Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa Uzinduzi wa Ujenzi wa Barabara ya Kibondo -Nyakanazi yenye urefu wa kilometa 54,Sherehe zilizo fanyika katika uwanja wa Standi Mpya ya Mabasi Kakonko katika mkoa wa Kigoma Rais yupo mkoani Kigoma kwa Ziara ya siku Tatu Baaadhi ya Viongozi wa vyama vya siasa na wananchi wa Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma wakisikiliza Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani...