Posts

Showing posts from January 19, 2017

MSANII NUH MZIWANDA AFUNGUKA MENGINE KUHUSU SHILOLE

Image
MSANII wa Bongo Fleva anayetamba na Wimbo wa Jike Shupa, Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ amesema kuwa japo kuna tetesi zinaenea mtaani kwamba amerudiana na aliyewahi kuwa mpenzi wake, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ suala hilo halina ukweli wowote ndani yake na wala hafikirii kabisa kurudiana na mwanadada huyo. Tetesi za Nuh kurudiana na Shilole zilianza kuvuma baada ya kusambaa kwa kipande cha video kilichowaonesha wakipatanishwa wakati wakiwa kwenye safari za Tamasha la Fiesta na watu kujiongeza kuwa wamerudiana. “Kilichotokea ni kwamba mimi na Shilole tumeondoa tofauti zetu za kibinadamu ambazo tulikuwa nazo baada ya kuachana. Lakini kuhusu kurudiana hahitakuja kutokea hata siku moja na siwezi kurudi nyuma kwenye hili maana nina mpenzi wangu ninayempenda,” alisema Nuh.

JAJI CHANDE: NAFURAHI KUUACHA MUHIMILI WA MAHAKAMA KATIKA HALI NZURI

Image
Jaji Mkuu Mstaafu Mohamedi Othman Chande amezitaka mahakama kufanya kazi kwa kuendana na kasi ya awamu ya tano pamoja na kufuata maadili ya taaluma ya sheria katika kutoa haki na sawa kwa wakati na kwa watanzania wote. Jaji Mkuu Mstaafu - Mohamed Chande Othman Jaji Chande ameyasema hayo mara baada ya kuapishwa kwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Prof Ibrahim Hamis Juma ambapo amesema kuwa kuongezeka kwa uwazi katika shughuli za mahakama kutasaidia sana katika kuendeshwa kwa kesi na kuamuliwa kwa wakati na watendaji wake. Amesema anafurahi anauacha muhimili wa mahakama katika hali nzuri huku akiwataka watendaji kuendeleza juhudi za kuboresha mifumo taratibu na sheria ili kutoa nafasi zaidi kwa kesi nyingi kushughulikiwa kwa haraka ikiwemo usikilizwaji wa kesi. Akizungumzia kuhusu mpango wa maendeleo wa miaka mitano ambao ameuacha amesema kuendelezwa kwa mpango huo kutasaidia kuharakisha usikilizaji wa kesi, kuongeza mfumo wa usikilizwaji wa kesi pamoj...

RAIS DKT MAGUFULI AMUAPISHA PROFESA IBREAHIM HAMISI JUMA KUWA KAIMU JAJI MKUU WA TANZANIA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Profesa Ibrahim Hamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Januari 18, 2018. Anayeshuhudia kushoto ni Jaji Mkuu mstaafu Mohamed Chande Othman.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo za kazi baada ya kumuapisha Profesa Ibrahim Hamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Januari 18, 2018.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpongeza baada ya kumuapisha Profesa Ibrahim Hamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Januari 18, 2018.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Katibu Mkuu Wizara ya Sheria na Katiba Profesa Sifuni Mchome na Naibu wake Mhe. Amon Mpanju...